Home Kimataifa Habib Kyombo aongezewa muda wa Mazoezi Afrika Kusini

Habib Kyombo aongezewa muda wa Mazoezi Afrika Kusini

10924
0

“Nimepokelewa salama hapa Pretoria. Nina furaha kuwa hapa na kila kitu kinaenda sawa. Jambo la utofauti hapa Afrika Kusini wamewekeza sana na wapo siriazi na mpira”

Hayo ni maneno ya Habib Kyombo ambaye yupo nchini Afrika Kusini kwa majaribio ndani ya klabu Mamelodi Sundowns.


Habib Kyombo yupo nchini Afrika Kusini ya siku 10 hivi leo amethibitsha kuwa ameongezewa muda wa kufanya mazoezi mengine zaidi kwa wiki moja.


“Nilifika hapa kwa muda wa siki 10. Nilifanya mazoezi na timu B kwa sasa klabu ilikuwa kwenye ratiba ngumu ya CAF na michuano mengine”

“Jana ilikuwa muda wa mazoezi yangu kukamilika. Lakini nikapewa taarifa kuwa kocha Mkuu Mosimame aliniongezea muda wa kufanya mazoezi kwa wiki nyingine”

Hata hivyo baada ya kufanya mazoezi kwa muda wa siku 10 Habib amepewa nafasi ya kuendelea kuonesha cheche zake zaidi. Mshambuliaji huyo hatari ambaye amefanikiwa kutwaa kiatu cha mfungaji bora wa Kombe la FA amekuwa na kiwango cha kuvutia.

Hajaweka wazi kuhusiana na mchakato mzima wa yeye kupata fursa ya kwenda kufanya majaribio hayo hadi pale mambo yatakapokamilika.


“Leo (Jumapili) nilipewa mapumziko na nimeambiwa kesho nitaanza mazoezi na timu ya wakubwa”

Bila shaka fursa ya yeye kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza ndiyo itakayompa nafasi ya kumshawishi Kocha Mosimane ili kumweleza raisi wa klabu hiyo Bwana Patrick Motsepe ili kuweza kumbakisha Kyombo ndani ya uwanja wa Loftus.

Hata hivyo kama mambo yataenda sawa kwake itakuwa fursa kwake. Klabu hiyo ina uhaba wa washambuliaji vijana. Katika Washambuliaji wake wengi wana umri mkubwa ispokuwa kijana mmoja mwenye miaka 20 na mwingine mwenye 27.

Jeremy Brockie
1987 (30) New Zealand
José Alí Meza
1991 (27) Venezuela
Phakamani Mahlambi
1997 (20) South Africa
Thokozani Sekotlong
1991 (27) South Africa
Cuthbert Malajila
Oct 3, 1985 (32) Zimbabwe
South Africa

 

Ikumbukwe Kyombo ambaye amezaliwa hapa Dar es Salam ana asili ya Bukoba kule Kanyigo ambapo ndipo chimbuko la wazazi. Habib alianzia maisha yake ya soka katika akademi ya BQ iliyopo maeneo ya Mbezi beach.

Alitumikia akademi hiyo kwa muda wa miaka 8 kabla ya kwenda Simba B. Aliwahi kucheza vilabu vya Lipuli Fc, Mbao Fc na kisha Singida United.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here