Home Kitaifa Habib Kyombo yupo Afrika Kusini kwenye majaribio na klabu kubwa nchini humo

Habib Kyombo yupo Afrika Kusini kwenye majaribio na klabu kubwa nchini humo

13294
0

Baada ya kung’ara na klabu ya Mbao Fc mshambuliaji Matata Habib Kyombo alinaswa na mabwenyenye wa Singida United kwa mkataba wa miaka mitatu.

Msimu wake wa kwanza amepata bahati ya kwenda nje ya nchi kwa ajili ya majaribio.

“Habib Kyombo amempata mwaliko wa siku 10 kwenda kufanya majaribio ndani ya klabu ya Mamelod Sundowns” Msemaji wa Singida alithibitisha hilo


Habib Kyombo kwa sasa yupo Africa kusini kwa ajili ya majaribio hayo. Klabu yake ya sasa Singida imesema ipo tayari kumruhusu mchezaji huyo kubakia afrika kusini kama atafanikiwa kubakia huko.

“Tumtakia baraka zote Habib. Tupo tayari kumruhusu kubaki klabuni hapo maana akifanikiwa yeye na sisi Singida tumefanikiwa” Alisema Festo Sanga.

Mamelodi Sundowns F.C.
Mamelodi Sundowns logo.svg
Majina Mamelodi Sundowns Football Club
Utani The Brazilians, Bafana baStyle, Masandawana, Kabo Yellow, Downs
Kuanzishwa 1970; Miaka 48 
Uwanja Lucas Masterpieces Moripe Stadium
Loftus Versfeld Stadium, Pretoria

 

Mamelodi Sundowns inapatikana katika jiji la Pretoria na inacheza Premier Soccer League yaani ligi kuu nchini humo. Klabu hiyo tokea ibadishwe kuwa PSL mwaka 1996 wametwaa ubingwa huo mara 8, na kufanikiwa kutwaa klabu bingwa ya afrika mwaka 2016 CAF (Champions League).

Kocha mkuu wa klabu hiyo Mosimane

Pia wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Nedbank Cup mara 4 na ni klabu pekee kutoka nchini humo kucheza michuano klabu bingwa ya vilabu.

  • CAF Champions League:
Nafasi Msimu
Mabingwa 2016
Nafasi ya pili 2001
  • CAF Super Cup:
Nafasi Msimu
Mabingwa 2017

 

Kama Habib atafanikiwa kubakia klabuni hapo basi atakuwa anacheza moja ya vilabu vikubwa nchini afrika kusini. Ataungana na Mtanzania mwingine Abdi Banda anayechezea klabu ya Baroka Fc.


Ikumbukwe kuwa Habib Kyombo msimu uliopita alipata mafanikio makubwa ikowemo tuzo ya mchezajj bora wa mwezi , akiwa anaitumikia wa Mbao FC, Habib Kiyombo alikabidhiwa kitita cha Tsh Milioni 1, Tuzo na King’amuzi kwa kuibuka Mchezaji Bora wa mwezi Desemba wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2017/2018. Akamaliza ligi na mabao zaidi ya 8 pia alikuwa mfungaji bora wa kombe la FA na alitajwa kwenye orodha ya wachezaji walio wania tuzo ya mchezaji bora wa msimu.

Klabu ya Mamelodi kwa sasa ina raia 7 wa kigeni mmoja kutoka Brazil, mwingine Marekani na mataifa mengineyo. Hata hivyo klabu hiyo pia iliwahi kuhusishwa na kuhitaji huduma za Abdi Banda


Usikose kutufuatilia maana tutakuletea mazungumzo ya moja kwa moja kutoka kwa Habib Kyombo kutoka Afrika Kusini. Kila la kheri Habib

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here