Home Kitaifa Haji Manara athibitisha Chama na Dida kuikosa Prisons kesho, Emmanuel Okwi naye...

Haji Manara athibitisha Chama na Dida kuikosa Prisons kesho, Emmanuel Okwi naye …

11696
0

Pazia la ligi kuu nchini Tanzania linatarajiwa kufunguliwa hapo kesho ambapo mabingwa watetezi klabu ya Simba Sc itakuwa uwanjani jijini Dar Es Laam kuikabili Prisons wanaosafiri kutoka mjini Mbeya.

Mchezo kati ya Simba na Prisons unatarajiwa kupigwa saa moja za usiku, na kuelekea mchezo huo msemaji wa mabingwa hao Haji Manara amezungumza na waandishi wa habari machache.

Kati ya machache ambayo Manara amaezungumza ni hali ya kiafya ya mchezaji Emmanuel Okwi ambaye alitolewa katika mchezo wao wa ngao ya hisani uliochezwa wikiendi iliyopita na kusema amekutana na madaktari wa timu na wamemuambia kuhusu Okwi.

Manara amesema mfungaji huyo bora wa ligi kuu msimu uliopita ana nafasi kubwa kuanza katika mchezo wa kesho na madaktari wamemthibitishia hivyo leo mchana.

Vile vile Manara ameweka wazi kwamba kiungo wao mpya Clatous Chama pamoja na golikipa wao mpya Deogratius Dida hawataweza kucheza mchezo huo kutokana na vibali vyao vya kuanza kufanya kazi kuchelewa(ITC).

Pia Manara amezungumzia mbio za ubingwa msimu huu, hii hapa video Manara akiongea kiundani kuhusu yote hayo mbele ya waandishi wa habari hii leo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here