Home Kimataifa HATARI: Deni la Juventus laongezeka mara mbili

HATARI: Deni la Juventus laongezeka mara mbili

12735
0
Juventus jana wametoa takwimu zao za mapato na matumizi ya mwaka ulioshia mwezi June. Repoti hiyo inaonesha kuwa deni la klabu hiyo limeongezeka mara mbili tofauati na hapo awali.

Deni hilo limefikia kiasi gani?

Deni la Mabingwa hao wa Serie A limeongezeka mpaka kufikia Euro milioni 309.8 sawa na $362M kutoka Euro milioni 162.5 za deni la mwaka uliopita.

Licha ya kubeba Serie A mara ya 7 mfululizo na kutolewa hatua ya robo fainali ya Uefa Juventus hali yao bado haijagangamala.


Vipi kuhusu faida na hasara walizopata?

Kutokana na deni lao kuwa kubwa hata faida waliopata pia imepungua hasa ukilinganisha na mwaka mmoja kabla. Baada ya kupata faida ya Euro milioni 42.6 kwa msimu wa 2016-2017, Juventus wametangaza kupata hasara ya Euro milioni 20 kwa msimu wa 2017-2018.


Kiungo wa klabu ya Juventus Sam Khedira ameongeza mkataba utakaomweka klabu hapo hadi 2021.


Mapato ya klabu nayo vipi?

Mapato ya klabu yalianguka kwa asilimia 10 kufikia mpaka Euro Milioni 504.7.


Mchanganuo kidogo 2017/18:
– Mapato = €504.7m
– Gharama za uendeshaji= €383.3m
– Malipo kwa madeni madogo na matumizi mengineyo= €122.8m
– Hasara baada ya kulipa kodi yote= €19.2m


Historia ya deni lao lipoje?

Juventus walikuwa na deni la Euro Milioni 90.7 likapanda kufikia Euro milioni 147.3 na sasa limefika 💶309.8M.

Sababu hasa za kuongezeka kwa deni hilo?

Inasemekana deni hilo liliongezeka kutokana

  • Gharama ngingi za usajili 💶119.5M,
  • Matumizi yasiyo ya lazima katika kuendesha michakato ya klabu.

Misimu ya awali klabu ilifaidika nini haswa kiasi cha kuwa na deni dogo na pato kubwa ukilinganisha na mwaka jana?

Msimu uliopita Juventus ilipata kiasi kikubwa cha fedha ambacho kwa sasa hawajakipata,

  • Kwanza walipata fedha nyingi walipofika fainali ya UEFA,
  • Pilli walipata takribani Euro 105M kutoka kwa mauzo ya Paul Pogba kwenda Manchester United.

Je deni hili limechangiwa pia na gharama za ujio wa Ronaldo?

Mabadiliko haya yanahusisha kipindi cha kuanzia June 30 mwaka jana mpaka June 30 mwaka huu wala haihusiani kabisa na usajili wao mkubwa na mkataba mnono wa Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid kwa Euro Milioni 100.


Je hadi ya klabu imepungua masokoni au bado mgonjwa anatafuniwa maji?

Klabu hii ya Turin hata hivyo thamani yake ilipanda baada ya Ronaldo, kwenye soko la hisa la Milan ambapo klabu hiyo fthamani yake ilifika Euro bilion 1.5.


Matarajio yao ni yapi?

Juventus wametabiri kuwa msimu 2018-19 huenda pia wakapaya hasara nyingine lakini wanaamini kufanya kwao vizuri katika michuano ya UEFA kutabadilisha upepo huo.

Kinachofuata ni nini?

Juventus chini ya mwenyekiti wao Andrea Agnelli pamoja na bodi ya wakurugenzi sasa wana kazi ya kupeleka ripoti hiyo kwa wanahisa wa klabu na kuwashawishi ili kulinda uwekezaji wa klabu hiyo. Ripoti hiyo inatarajiwa kuwasikishwa mwezi wa 10.


Ratiba ya Juventus wikiendi hii na kuendelea.

Septemba, 2018
Tarehe
16
JUV
SAS
4:00 PM ligi
19
VAL
JUV
10:00 PM UEFA
23
FRO
JUV
9:30 PM ligi
26
JUV
BOL
10:00 PM ligi
29
JUV
NAP
7:00 PM ligi
Oktoba 2018
Tar
2
JUV
BOY
7:55 PM UEFA
6
UDI
JUV
7:00 PM ligi
20
JUV
GEN
7:00 PM ligi
23
MAN
JUV
10:00 PM UEFA
27
EMP
JUV
7:00 PM ligi
Novemba 2018
Tarehe
3
JUV
CAG
10:30 PM ligi
7
JUV
MAN
11:00 PM UEFA
11
MIL
JUV
10:30 PM ligi
24
JUV
SPAL
8:00 PM ligi
27
JUV
VAL
11:00 PM UEFA

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here