Home Ligi EPL Hatimaye Heung Min Son akwepa kwenda kulitumikia jeshi

Hatimaye Heung Min Son akwepa kwenda kulitumikia jeshi

11720
0

Kama kuna mwanasoka ambaye leo ilokiwa siku yake kubwa ya furaha baasi ni nyota wa Tottenham Hotspur na timu ya taifa ya Korea Heung Min Son.

Heung aliiongoza timu yake ya taifa kuipiga Japan kwa mabao 2 kwa 1 hii leo na kutwaa ubingwa wa michuano ya Asian Games kwa mwaka huu.

Furaha ya Son hii leo haikuja kutokana na ushindi wa leo bali furaha kubwa zaidi ni baada ya kufanikiwa kwenda kulitumikia jeshi la nchini kwao kwa miaka miwili.

Ikumbukwe kwamba kama Korea wangeshindwa kupata ushindi hii leo, Son na baadhi ya wenzake ingewabidi waende kulitumikia jeshi kutokana na umri wao.

Lakini kama mwanamichezo amelifanyia taifa jambo kubwa ikiwemo kombe lolote au medali ya dhahabu baasi nchi humsamehe kwenda kutumikia jeshi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here