Home Kimataifa Hatimaye “Kane The Big Machine” wa WWE ashinda uchaguzi nchini Marekani

Hatimaye “Kane The Big Machine” wa WWE ashinda uchaguzi nchini Marekani

17915
0

“Kane ni mdogowake The Under Taker” umeshawahi kusikia hiyo kauli katika mieleka? Nina uhakika umeshasikia na ukaamini kama nilivyoamini mimi na kama uliamini sasa nakuambia SIO KWELI.

Wengi wetu tangu tukiwa wadogo tulikuwa tukiamini Kane na Undertaker ni ndugu kutokana na ukaribu wao katika mieleka lakinj vile vile kutokana na mionekano yao lakini kumbe kiuhalisia hawana hata undugu.

Okay tuachane na Under Taker tumzungumzie Kane, ni hivi hii ilikuwa wiki njema kwa nyota huyo wa mchezo wa mieleka baada ya kufanikiwa kushinda cheo cha Umayor katika mji wa Tennessee nchi Marekani.

Kane ameshinda jimbo hilo ambapo alikuwa akigombea kupitia chama cha Republican kwa kupata kura 51,804 ambayo ni sawa na asilimia 66, akimshinda mgombea wa Democratic aitwaye Lina Hanney.

WWE walitumia akaunti yao ya Twitter kutoa pongezi kwa Kane ambaye jina lake halisi ni Glenn Jacobs kwa kuandika “Hongera Kane kwa ushindi wako wa umeya wa Knox Country mjini Tennessee”.

Raia mbalimbali wa Tennessee wamepokea ushindi huo kwa hisia tofauti lakini wengi wakisema wanatawaliwa na wanamieleka, kwani raisi wa nchi hiyo Donald Trump aliwahi kujihusisha na mieleka na sasa meta wao ni Kane.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here