Home Kitaifa “Hatuna presha, presha ipo kwa Vita”-Aussems

“Hatuna presha, presha ipo kwa Vita”-Aussems

2649
0

Kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika Simba vs AS Vita, kocha mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema wao hawana presha bali presha ipo kwa wapinzani wao.

“Mimi nipo sawa na vivyohivyo kwa wachezaji wangu wapo vizuri, ni mechi yenye msisimko sana tunajua tukishinda tutaingia robo fainali na tumesubiri jambo hili kwa miezi 7 sasa.”

“Hata kama matarajio hayakuwa makubwa sisi kufika mbali kwenye ligi ya mabingwa Afrika, lakini bado tuna nafasi kwa hiyo hatuna presha, zaidi presha ipo kwao (AS Vita) kwa sababu ni wanafainali wa kombe la shirikisho mwaka jana na kama hawatafuzu itakuwa jambo baya sana kwao.”

“Hatupo katika hali inayofanana, chochote kitakachotokea ni ziafa kwetu, tuna nafasi adimu ya kucheza mchezo huu muhimu mbele ya mashabiki 60,000 kwa hiyo itakuwa mechi nzuri na wachezaji wapo tayari.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here