Home Kimataifa Hili zigo Cannavaro alilompa “Ninja” ni kubwa ila wazungu hawatoi

Hili zigo Cannavaro alilompa “Ninja” ni kubwa ila wazungu hawatoi

11477
0

Nadir Haroub “Cannavaro” amestaafu soka, huyu ni mlinzi bora wa kizazi cha sisi vijana tuliowahi kuzaliwa miaka ya tisini naa. Nadir ni nahodha haswa na amestahilu kweli kuagwa kwa heshima.

Jezi namba 23 aliyokuwa anaivaa, Yanga waliamua kuistaafisha lakini mwenyewe amekataa na zigo hilo amempa Ninja ambaye msimu ujao ndiye ataanza kuvaa jezi namba 23.

Nimejaribu kuangalia tukio kama hili la kustaafisha namba kwa wenzetu wazungu, lakini nimegundua mara nyingi wao hawatoi namba kwa watu, ikistaafishwa wanakubali.

Javier Zanetti. Inter Milan waliamua kustaafisha jezi namba 4 ya Muargentina huyu mwaka 2014 kama heshima ya aliyoifanyia timu yao na Zanettu akapokea heshima hiyo, Zanetti aliichezea Inter michezo 625 na kufunga mabao 61.

Paulo Maldini. Miaka 25 akiwa na Ac Milan alishinda Champions League 5, kombe la klabu bingwa dunia na Serie A 5 hii iliwafanya Ac Milan kustaafisha jezi namba 3 mwaka 2009 kama heshima kwa Maldini.

Diego Maradona. 1984 alijiunga na klabu ya Napoli akitokea Barcelona, ambapo akiwa Napoli alifunga mabao 81 kwenye michezo 188 na kutwaa Serie A, UEFA Cup, Coppa Italia na Super Copa Italiana hii ikawafanya Napoli kustaafisha jezi namba 10 mwaka 1991.

Kobe Brayant. Huyu ni katika NBA na yeye alikuwa akivaa 24 japo aliwahi kuvaa pia jezi namba 8 lakini aliposema anastaafu timu yake ya Los Angeles Lakers iliamua kustaafisha jezi zote mbili 8 na 24

Lakini kuna huyu Aldair nyota wa zamani wa Brazil na As Roma alivaa namba 6 baadae ikastaafishwa 2003, lakini Mholanzi Kelvin Strootman alipofika Roma aliiomba hiyo namba na Roma wakawasiliana na Aldar aliyekuwa Brazil akakubali irudishwe.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here