Home Kimataifa Hispania waidhalilisha Croatia, huku Lukaku na Rashford wakitakata

Hispania waidhalilisha Croatia, huku Lukaku na Rashford wakitakata

13437
0

Dakika 35 tu za kipindi cha kwanza zilitosha kuona aibu inayokuja kwa timu ya taifa ya Croatia katika mchezo wao wa leo zidi ya timu ya taifa ya Hispania kwenye michuano ya UEFA Nations League.

Dakika hizo 35 ilikuwa tayari Saul Niguez, Marco Asensio na bao la kujifunga la Lovre Kalinic yaliufanya mchezo kwenda half time kwa Hispania kuongoza kwa mabao 3-0.

Croatia walirudi kipindi cha pili wakiwa na juhudi ya kutafuta kuchomoa lakini tabu ikawa pale pale baada ya kufungwa 3 zingine na kuwa 6 huku safari hii wafungaji wakiwa Rodrigo, Sergio Ramos na Isco.

Hiki ndio kipigo kikubwa zaidi kwa Croatia kuwahi kukipokea na wengi wameshangazwa kwa namna walivyotepeta hii leo haswa ukizingatia kwamba hawa ni washindi wawili wa michuano ya kombe la dunia.

Katika mchezo mwingine Eden Hazard na Romelu Lukaku walifunga mabao mawili kwa timu ya taifa ya Ubelgiji na kuwafanya kuibuka kidedea kwa mabao 2-0 zidi ya Iceland.

Kipindi cha pili Romelu Lukaku alifunga bao la 3. Kwa mabao haya ya Lukaku na Hazard sasa wanakuwa wamefunga mabao 30 kwa pamoja katika michezo 19 tangu mwanzo wa msimu uliopita katika timu ya taifa.

Lakini pia kulikuwa na mchezo wa kirafiki kati ya timu ya taifa ya nchini Uingereza ambao walikuwa wakikipiga zidi ya timu ya taifa ya Switzerland.

Marcus Rashford alifunga bao pekee kwa timu ya taifa ya Uingereza na hii inamfanya kufunga kwa mara ya kwanza katika michezo miwili mfululizo ya timu ya taifa ya Uingereza.

Katika mchezo huu pia kinda Ben Chilwell aliingia uwanjani dakika ya 77 na kumfanya kuwa mchezaji wa 12 chini ya miaka 21 kuichezea Uingereza chini ya utawala wa Southgate.

Lakini vile vile Chilwell amekuwa mchezaji wa kwanza kuichezea timu ya taifa ya Uingereza katika uwanja wa nyumbani wa klabu yake (uwanja wa Leicester) tangu mara ya mwisho Paul Scholes kufanya hivyo 1997(Old Traford).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here