Home Kimataifa Hivi mnamkumbuka Louis Saha?

Hivi mnamkumbuka Louis Saha?

4977
2

Louis Laurent Saha, amezaliwa mwaka 1978 nchini Ufaransa, sasa akiwa na umri wa miaka 39 pia amewahi kuichezea timu ya Taifa Ufaransa, ameichezea michezo 20 na kufunga mabao 20 tu.

Nyota huyo alianzia maisha yake ya soka katika kituo kimoja cha academy, kilichokuwa kinaitwa Metz, na baadaye alijiunga na klabu ya Newcastle, kwa mkopo msimu wa mwaka 2000-01 alijiunga na klabu ya Fulham, ambayo ilikuwa inacheza ligi daraja la Kwanza na kuipandisha ligi kuu England msimu wa Kwanza.


Sasa ni rasmi. Ramsey leo atafanya vipimo vya afya huku akitarajia kujiunga na Juventus mwezi June wakati mkataba wake na Arsenal utakapotamatika.


Msimu wa mwaka 2002-03 klabu ya Manchester United, ilimsajili kwa kiasi cha paundi milioni 12.4 kutoka katika klabu ya Fulham.

Hata hivyo Saha, akuwa na wakati mzuri ndani ya klabu ya Manchester United, baada ya kukumbuna na majeraha ya mara kwa mara.

Mshambuliaji huyo aliitumikia klabu ya Manchester United, kuanzia msimu wa mwaka 2004-08 alifanikiwa kutwaa mataji mawili ya ligi kuu na kombe la ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, pia alifunga mabao sita kwenye michuano ya kombe la ligi.


Vipigo vizito alivyotoa man city msimu huu akiwa nyumbani Ethad.

Man city 9-0 Burton
Man city 7-0 Rorthenham
Man city 6-0 Shakhtar D
Man City 6-1 Southamptom
Man City 5-0 Burnley
Man City 6-1 Huddersfield


Baada ya kuitumikia klabu ya Manchester United, misimu minne na nusu klabu ya Everton, walimsajili msimu wa mwaka 2008-12 aliichezea michezo 97 na kufunga mabao 27.

Msimu wa mwaka 2012 alijiunga na klabu ya Tottenham, akiwa mchezaji uhuru ameichezea michezo 10 na kufunga mabao 10 tu.

Pia amewahi kuitumikia timu ya Taifa Ufaransa, kwenye michuano ya kombe la mataifa mwaka 2004 na akiwemo kwenye kikosi cha Ufaransa, kilichocheza fainali ya kombe la dunia mwaka 2006.

By Azizi Mtambo 15

Comments

comments

2 COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here