Home Ligi EPL Hongera Haji Manara kwa ushindi lakini kwa hili la Shaffih Dauda umepayuka

Hongera Haji Manara kwa ushindi lakini kwa hili la Shaffih Dauda umepayuka

19523
1

Jana mabingwa wa soka nchini Tanzania klabu ya soka ya Simba Sc ilifanikiwa kutwaa ngao ya hisani katika mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar uliochezwa pale Kirumba Mwanza.

Magoli mawili kutoka kwa Meddy Kagere na Hassan Dilunga yalimpa mnyama ngao hio na Simba walistahili ubingwa haswa kutokana na uwekezaji wao waliowekeza msimu huu.

Baada ya mechi kuisha usiku watu wa soka walijumuika sehemu mbali mbali Mwanza kusherehekea ubingwa wa Simba na Shaffih Dauda alikuwepo viwanjani usiku akitinga jezi ya Mtibwa Sugar.

Baada ya picha ya Shaffih kuvaa jezi ya Mtibwa maneno yaliibuka mengi kuhusu uhalali wa mchambuzi huyu wa soka kuvaa jezi ya timu fulani wakati yeye ni mchambuzi na hapaswi kuwa na timu.

Moja ya watu waliohoji suala hili ni msemaji wa mabingwa wa nchi Haji Manara, Haji anasema “najiuliza kama mwanahabari ambaye umefikia level za kupewa ukuu wa vipindi kisha ukajipambanua kwa kuvaa jezi ya timu nyingine ,utapataje uhalali kuichambua mechi hiyo au utaweza kuizungumzia vyema timu pinzani?, kwangu mimi ni un proffesional”

Nikajiuliza Haji aliandika hii comment akiwa viwanjani usiku ule? Haji ana uzoefu mkubwa katika soka lakini kweli anaweza kuhoji hili? Kuvaa jezi ya timu ndio kuishabikia? Na kuwa shabiki wa timu fulani ndio hupaswi kuchambua kuhusu timu nyingine? HAPANA.

Kwanza Shaffih sijui mimi kama ni mshabiki wa Mtibwa, Coastal, Simba au Yanga, kuvaa jezi haimaanishi wewe ni mshabiki wa timu fulani. Kuna wakati mtu anavaa jezi kwa mapenzi ya mchezaji fulani, kama kuvaa jezi na ushabiki baasi Dauda anashabikia timu zaidi ya 100 duniani kutokana na jezi zake.

Lakini pia kuwa shabiki wa timu fulani haikuzuii na haikunyimi hiyo legitimacy/uhalali wa kuchambua mechi ya wapinzani na sio UNPROFESSIONAL kama Manara unavyosema, ninawajua wachambuzi wakubwa kabisa wa soka ambao ni mashabiki kindaki ndaki wa timu fulani duniani na wanachambua soka katika mashirika makubwa na yenye heshima kubwa katika soka.

Garry Neville. Kuanzia 1993 hadi 2012 ameichezea Manchester United , lakini kwa sasa ni mchambuzi maarufu duniani katika kituo cha Sky Sports na amekuwa moja ya wachambuzi mashuhuri dunianj, Sky Sports nao ni un profesional kumuajiri mtu ambaye ni shabiki wa timu fulani.

Thiery Henry. Pamoja na kuichezea Barcelona lakini watu wote wanafahamu huyu ni mfuasi wa Arsenal na pia ni kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Ubelgiji lakini bado ni mchambuzi wa soka.

Frank Lampard. Lampard naye kama wenzake hapo juu, achilia mbali kuichezea Chelsea lakini huyu ni mshabiki mkubwa wa klabu hiyo na bado anachambua mechi za Chelsea dhidi ya timu nyingine.

Garry Lineker. Moja ya wachambuzi maarufu duniani ni Lineker akifanya kazi na BT SPORTS,BBC na mashirika mengine makubwa ya habari, lakinki Lineker humuambii kitu kuhusu Leicester City hata walipobeba ubingwa alivua nguo kwa furaha na bado anaiongelea EPL kiuhalali.

Rio Ferdinand. Mshabiki kindaki ndaki wa Manchester United lakini akiwa Bt Sports Ferdy huwa anasahau kuhusu United na anawapiga haswa lakini wakishinda anashangilia, huyu naye vipi.

Comments

comments

1 COMMENT

  1. Hao aliotaja mwaandishi wa hii makala atuambie ni Lini aliwaona wanachambua na wamevaa jezi za timu pinzani anazochambua? Au kutangaza?… Maana mifano yake yote haiendani na hoja.. Mwandishi wa hii kitu “Go back to class again”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here