Home Kimataifa Huku Ole Gunnar kule Harry Kane

Huku Ole Gunnar kule Harry Kane

3388
0

Tottenham Vs Manchester United, mchezo huu utapigwa katika dimba la Wembley Stadium, majira ya saa 19:30 usiku.Tottenham wanaangalia uwezekano wa kushinda michezo mitatu mfululizo dhidi ya Manchester United, mara ya mwisho kufanya hivo ilikuwa mnamo mwezi September 1960.Manchester United, wamepoteza michezo mitatu ya mwisho ugenini katika ligi kuu England dhidi ya Tottenham, na katika michezo 23 waliyokutana kwenye michuano yote kuanzia mwaka 1992 mpaka mwaka 2014 ameshinda michezo 12 na sare 8.Tottenham, inaweza kuwa timu ya Kwanza kushinda michezo minne mfululizo dhidi ya Manchester United, mara ya mwisho ilikuwa Everton, mnamo mwaka 1987 alishinda michezo minne katika uwanja wa nyumbani.Manchester United, wamepoteza michezo miwili kati ya michezo mitatu ya mwisho katika dimba la Wembley, na ukijumuisha na mchezo wa msimu ulipoita katika michezo 15 ameshinda michezo 8 sare 5 na amepoteza 2.Manchester United, wameshinda michezo minne kati ya michezo 17 ya ugenini kwenye ligi kuu England dhidi ya timu zinatoka mji wa London, amepoteza 9 na sare 4.Tottenham, mara ya mwisho kupoteza michezo miwili mfululizo katika uwanja wa nyumbani ilikuwa mnamo mwaka 2015 alipoteza dhidi ya Aston Villa, na Manchester City.Baada ya kushinda michezo minne ya ligi kuu msimu uliopita dhidi ya timu kubwa sita za juu Manchester United, katika michezo mitano msimu huu dhidi ya timu sita kubwa za juu ajashinda mchezo hata moja amepoteza 3 na sare 2.Harry Kane, amefunga mabao 8 katika michezo 8 ya ligi kuu michezo aliyoanza.Sanchez, akiwa na timu ya taifa na klabu kwa ujumla kwenye michuano yote amehusika katika upatikanaji wa mabao 9 katika michezo 9 katika uwanja wa Wembley amefunga mabao 8 na assist 1.Rashford, amehusika katika upatikanaji wa mabao 9 katika michezo 8 ya ligi kuu akiwa na Manchester United, amefunga mabao 4 na assist 5 pia anaangalia uwezekano wa kufunga katika michezo mitatu mfululizo kwa mara ya Kwanza katika maisha yake.@Azizi _Mtambo_15

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here