Home Uncategorized Huyu Chama na Aussems wanatupatia somo

Huyu Chama na Aussems wanatupatia somo

7385
0

Na Robert KombaTumeshuhudia soka la kiwango kikubwa toka kwa Simba sports club ikicheza na Mbababe Swallows ugenini huko nchini Eswati (Swaziland). Zaidi ya matokeo ya kupendeza kwa upande wa simba ishinda 4-0, tumeweza kuona kwa uzuri zaidi, nadharia ya uchezaji wa simba sports club chini ya mwalimu Mbelgiji Aussesms.Simba katika mechi hiyo walitumia mfumo wa 4-2-1-3, muundo(formation) ambao kwenye karatasi ulionekana kama 4-3-3 ambapo golini alikuwa Tanzania one Aishi Manula, mabeki (Gyan, Wawa, Nyoni, M. Hussein) viungo wawili wanao “hold” timu (Kotei, Mkude) kiungo mmoja wa ushambuliaji ambaye pia alipewa nafasi huru ya kucheza (Chama) na washambuliaji watatu (Kagere, Bocco na Okwi) .

Kikosi ambacho kwa kiasi kikubwa ndio kimekuwa kikianza katika mech za simba kwa hivi karibuni na mabadiliko pekee yakiwa ni Kichuya ambaye huchezeshwa kama sehem ya viungo wa kati na Kotei kuanzia benchi.Tofauti na mechi ya mzunguko wa kwanza iliyofanyika hapa Tanzania, Aussems aliutaka mstari wake wa kwanza was ulinzi ambao ni washambuliaji watatu wa mbele, kuacha kukabia juu na badala yake kusogea nyuma ili kuweza kufanya mistari ya ulinzi kuwa karibu, na hiyo kuwapa ugumu mbabane katika kushambulia.

Hii iliweza kuwaacha Mbabane wajenge mashambulizi kutokea nyuma, lakini walifeli kupenya ngome ya simba na walipokuwa wakikaribia eneo la katikati, simba walifanya pressing na kuanza kushambulia nafasi iliyoachwa nyuma na mabeki wa Mbabane. Mashambulizi ya simba walikuwa hatari kwani walitumia uwezo wa kukokota mpira kwenye nafasi finyu wa kiungo Clautos Chama ambaye alikuwa ni wa kwanza kulishambulia eneo hilo na kuonekana kama anacheza false 9.

Chama alikuwa kivutio kikubwa na akiutumia Uhuru wake uwanji vizuri kwa kuchagua sehemu yenye mapungufu (nafasi ya kutosha) katika ngome ya wapinzani na kushambulia, na kuwapa ugumu mabeki wa Mbabane kwani washambuliaji wa simba pia waliliacha wazi eneo la ushambuliaji kitu kilicho wachanganya zaidi. John Bocco ambaye alianza kama mshambuliaji wa kati, alionekana pembeni Mara nyingi na alkadharika Kagere na Okwi, hakuna mmoja kati yao aliyekaa katika eneo la ushambuliaji kwa muda mrefu, ilikuwa ni kitu cha kuvutia na imeonyesha ubora wa simba sio tu kwa ubora wa wachezaji, lakini pia mbinu nzuri za mwalimu katika kujaribu kupata kilicho bora kutoka kwa wachezaji wake wote bora.

Hivyo namna mwalimu Patrick Aussesms alivyomtumia Chama na wazo zima la Pressing ni kitu cha kujifunza sana kwa walimu wa nyumbani, lakini pia wadau wa soka ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakiwekeza kujua ubora wa wachezaji na figisu za nje ya uwanja kuliko mbinu na utumiaji wa wachezaji hao. Mbinu hizi kutoka kwa mgeni zinaweza kutuletea mabadiliko katika soka Leo kama ambavyo tumeona soka la uingereza likibadilishwa na ujio wa wachezaji kama Eric Cantona.

Alicheza shimoni katika kikosi cha Leeds kisha Manchester united katika miaka ya 90 na kisha timu nyingi za uingereza kusajili wachezaji wa namna hiyo kama Denis Bergkamp, Zola, Ted Sherringham na Juninho pernambucano ambao wamesaidia sana kubadili falsafa ya Soka la Uingereza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here