Home Ligi EPL Huyu kinda wa Arsenal taarifa zake tunazo, ni suala la muda tu

Huyu kinda wa Arsenal taarifa zake tunazo, ni suala la muda tu

13945
0

Leo nimekutana na bango la kinafiki sana. Kuna mdau kaniambia eti “Nimegundua Wenger ameacha pengo”

Mantiki yake ni kwamba eti Unai ni mbovu tu sawa na Wenger. Mimi nimeona baadhi ya watu wakiwakejeli Arsenal na Mabango ya Wenger In wakimaanisha wanamhitaji Wenger arudi.

City bado ni wale wale wameanza kama walivyomaliza msimu uliopita sio kwa sababu tu ni mabingwa ila hata aina yao ya uchezaji kuanzia kipa mpaka waliopo benchi. Wamepikwa wameiva vizuri.

Tuachane na hayo.

Kuna bwana mdogo mmoja amenikosha sana namna alivyojiamiani. Alikuwa na nywele nywele kichwani hivi alikuwa akicheza pembeni ya Xhaka.

Lakini pia nimegundua kuna watu wa aina kadhaa. Wapo wanaoangalia lakini hawaoni vizuri na wapo wanaoona ila hawaangalii vizuri.

Kuna wale watu wanamuona mchezaji uwanjani lakini hawamwangalii anachokifanya, wanasubiria kuona tukio baya au zuri ndipo wamuangalie vizuri. Tena wanaweza kumuadhibu mchezaji kwa tukio moja tu wala wasihangaike kumuangalia tena.

Kuna wale watu wanamuangalia mchezaji uwanjani lakini hawaoni kile anachokifanya kwa sababu labda wanakwenda na mawazo yao kichwani (Yaani yeye akili yake timu fulaninifungwe tu hata kama kuna mchezaji amefanya vyema huo upande yeye haimhusu, tena ole wake akosee)

Huyu Guendouzi wengi kuna watu wamemuona kwa jicho moja kwa sababu labda tu walitaka kuona Arsenal inafungwa 4 au wengine walitaka kuona Arsenal ikishinda hivyo kosa moja la huyu bwana mdogo kwao ni nongwa na waanamininkuwa ndiye chanzo cha Arsenal kufeli leo.

Guendouzi amecheza mechi yake ya kwanza. Akitokea huko Ufaransa. Mbaya zaidi anakutana na mabingwa na wachezaji ambao tayari wameelewana na ni wazoefu wa ligi (Fernandinho, Ilkay na De bruyne). Pembeni yake alikuwepo Xhaka na Ramsey ambao wote wamecheza kwa kiwango cha kawaida sana hasa ukilinganisha uwezo walio nao.

Guendouzi ndiye mchezaji pekee wa ndani wa Arsenal aliyemiliki mpira kwa kiwango kikubwa zaidi akiwa na alama 4.7, Ozil 4.0, Ramsey 1.1, Aubameyang 2.1, Xhaka 4.4, Micky 3.2.

Kuna wanafiki wamekaa pembeni wanasema eti Gue alikuwa anaongoza kwa kupoteza mipira zaidi. Sio tatizo sana endapo kama haikuwa na madhara kwa timu.

Kuhusu kutoa maboko. Sawa Gue amepoteza pasi 7, akifuatiwa na Ozil aloyetoa fyongo pasi 5, pia yupo Sterling amepoteza nae pasi 7,Aguero pasi 5, Gundogan pasi 4, n.k. labda tuseme ni kule kutokujiamini jasa ukiangalia huu n mchezo mkubwa na mgumu kwake hasa ugeni wake nao ulichangia.

Narudia tena kusema kuna watu wanakodoa macho kwenye TV lakini hawaoni. Wao wanaona makosa tu.

Ukiangalia takwimu zinaonesha hakuna kiungo aliyemzidi Gue kwa pasi zilizokamilika. Gue ana wastani wa pasi zilizokamilika kwa asilimia 81 akiwa sawa na Xhaka. Ozil 78, Auba 70, micky 77, Ramsey 64 yaan huyu ndiye aliyeongoza kwa kutoa pasi fyongo zaidi kuliko mchezaji yeyote wa Arsenal lakini haongelewi. Mchezaji pekee aliyemzidi ni Mustafi mwenye 90.

Wanasema hachezeshi timu vyema. Ukiondoa Maitland Niles hakuna mchezaji aliyemzidi Gue kwa kukokota mipira. Belerini Ramsey, Gue, wote wamekimbia na mpira mara mbili. Huyu ndiye aliyepiga mpira mirefu mara tano na yote kukamilika kwa ufasaha zaidi nyuma ya Xhaka aliyepiga mara 7. Hakuna mchezaji mwingine aliyemzidi zaidi ya Xhaka.

Amefanikiwa kupiga pasi zilizoelekea mbele mara 27 akizidiwa pasi moja tu na Xhaka mara 28. Huyu ndiye mchezaji aliyeanzisha mashambulizi ya haraka kutokea katikati ya uwanja mara 19 idadi kubwa zadi kuliko mchezaji yeyote wa Arsenal.

Mlitaka afanyeje? Ndipo mumuone bora. Licha ya kwba ametumika zaidi dimba la kati lakini pia aliweza kupiga pasi 11 katika eneo la ulinzi la Man City.

Kuhusu kukaba.

Kuna ule mfumo wa ukabaji kwa kutelezea mguuni mwa mpinzani wako kwa sisi wazungu tunaita takolini au wakenya wanasema manowari au msambamba. Gue amezidiwa takolin na mchezaji mmoja tu ambaye ni Micky. Amecheza takolini mara 4, huku Micky akicheza mara 5. Xhaka 2, Ramsey 1, Ozil 1, Mustafi 4, Belerin 2, Sokratis 2. Sasa unasemaje hakabi?

Arsenal wameharibu mipira ya wapinzani wao mara 14 huku Belerin akifanya hivyo mara 5 akiwafuatiwa na Gue mara 4, na Mustafi mara 3, Xhaka na Ramsey wote hawajafanya jaribio lolote lililozaa matunda. Ni viungo wawili tu waliofanikiwa kuondosha mpira katika eneo la hatari Gue na Xhaka wote mara moja. Gue hajazidiwa na mchezaji yeyote katika kubloku mipira. Amebloku mara 2 na Xhaka mara 2 pia wengine wote pamoja na mabeki wamebloku mara moja moja.

Gue amenyang’anywa mpira mara moja tu. Hakuna anayejali kama Gundogan amenyang’anywa mipira mitatu, hakuna atakayekwambia kama Sterling amepoteza mipira mitano ila utaambiwa yupo Guendzou amecheza utumbo. Utumbo ni wewe unayetazama na huoni.

Mkongwe Ian Right ansema, “Gue ana miaka 19 lakini ameonesha ukomavu wa miaka 30. Anapoteza mpira wala haogopi anaendelea kupambana na kila mara bado ana utaka mpira”

Watu hawatamuongelea Xhaka aliyeharibu pasi mara 19 ila watalalamikia mpira ambao Gue aliukadiria kimakosa. Swali la kwanza linakuja hapa, Gue alikadiria mpira wa juu kwa lengo la kuiondosha kwa bahati mbaya mpira ukadunda vibaya, cha ajabu nyuma yake hapakuwepo na beki yeyote yule ikiwa yeye alikuwa hatua 15 kutoka katikati ya uwanja. Namba 4 na 5 walikuwa wapi? Hata kama bao lingefungwa hatuwezi kusema moja kwa moja kwamba ni uzembe ilihali yeye alijitahid kucheza mpira ukamshinda vipi walinzi wa nyuma wako wapi?

Kuhusu bao la Sterling wakati mwingine tuwasifie na wapigaji.. Hakuna aliyedhani kama Sterling angeweza kujikunja kiasi kile. Belerin mwenyewe alimzuia kwa muda kabla hajaachana nae. Tunaweza kusema kimsingi kama Belerin alihangaika nae na hakuweza kumpokonya mpira basi na mfungaji apongezwe.

Gue amegusa mpira mara (72) zaidi ya mchezaji yeyote wa Arsenal, Mustafi (57), Xhaka (55) na Ozil (55). Amecheza pasi mara (47) zaidi ya mchezaji yeyote wa Arsenal , Xhaka (44) na Ozil 40..
na amechezewa faulo mara 3 zaidi ya mchezaji yeyote wa Arsenal.

Hii ni lulu kwa baadae. Huyu kijana akiendelea kuaminika hapo baadae mtaongea lugha tofauti.

Mechi ya leo amekuwa mgeni tu. Matteo Guendouzi mechi hake ya mwisho ya ushindani alicheza ligi dafaja la pili (French 2nd division) kati ya Lorient na Valenciennes, mbele ya mashabiki 8,000. Leo akiwa na miaka 19 amekutanishwa na Manchester City mbele ya mashabiki 60,000 halagu atakuja mwanaume wa dar atakwambia kacheza hovyo.

Na Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here