Home DOKUMENTARI Huyu Klopp ataikomboa Liverpool kweli kwa mfumo wake?

Huyu Klopp ataikomboa Liverpool kweli kwa mfumo wake?

9740
0

Na Robert Komba

Mwanzoni mwa msimu wa 2018/19 katika ligi kuu ya uingereza, Liverpool pamoja na Manchester city ndizo timu zilizokuwa zikipewa nafasi kubwa ya kuchukua ubinwa katika msimu huu. na hiyo ilitokana na sajili zilizofanywa na timu hizo, sajili ambazo zilionekana fika zinakuja kuzikamilisha timu hizo. Na haishangazi sana kuona hadi sasa ikiwa theluthi moja ya ligi ikiwa imechezwa, timu hizo zikishindana katika nafasi ya kwanza na ya pili kwa tofauti ya alama 2 tu. Lakini zaidi hayo, kiwango cha Liverpool kimekuwa kikitiliwa mashaka na baadhi ya watu ikiwemo mimi.

Kops tayari wameshatolewa katika kombe la ligi (capital one cup) na wana uwezekano mkubwa wa kukosa nafasi ya kufuzu 16 bora ya ligi ya mabinwa barani ulaya. Na ijapokuwa wamepata droo katika mech 3 kati ya 4 walizocheza na timu sita za juu bado hawakuitawala michezo hiyo kwa namna iliyotarajiwa.

Nguvu ya Liverpool ni uwezo wa wa kufanya mkazo (pressing) katika eneo la juu ya uwanja, mtindo ambao unajulikana kama gegenpressing. Kimbinuu, mpira wa miguu umegawanyika katika hatua nne uwanjani nazo ni 1. Kushambulia (attack) 2. Kuzuia (defence) lakini katika mpira wa kisasa (modern football) tunaweza kuungalia vipindi viwili zaidi navyo ni vipindi vya mpito (transitions) 3. Kipindi cha mpito kutoka kushambulia kwenda kuzuia (transition to defence) na 4.

Kipindi cha mpito kutoka kuzuia kwenda kushambulia (transition to attack). Wadau wengi wa soka ulimwenguni pamoja na Pep Guardiola wanakiri kuwa Liverpool katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita imekuwa timu bora zaidi katika vipindi vya mpito (transitions). Kiwango kikubwa walichokionyesha msimu uliopita na hadi kufikia fainali ya ligi ya mabinwa kiliashiria Liverpool imerudi kuwa moja ya timu bora ulaya ikijulikana zaidi kwa style hiyo ya Geggenpressing.

Na mabadiliko ya usajili wa beki golikipa Allison Becker, Virgil van Dijk, viungo Naby Keita na Fabinho, pamoja na winga Shedran Shaqiri yaliashiria mambo mazuri yanakuja kwa upande wa Liverpool. lakini hadi sasa haishangazi sana kusikia mtu akisema Liverpool wamekosa kuyafanya tuliyoyatarajia kwa kiasi fulani.

Liverpool haijawa timu inayotawala michezo mikubwa hasa ikiwa na mpira, ambapo katika nyakati tofauti imeshafungwa na Napoli, Chelsea na PSG. shida hii imekuwepo kwa kipindi kirefu sasa na hata sajili za keita na shaqiri ziliashiria kuwa sasa klopp anataka kutenengeza timu ambayo sio itakuwa tegemezi kwenye kulazimisha magoli kwa kukabia juu, bali pia itaweza kutengeneza nafasi za magoli ikiwa na mpira.

Lakini bado naiona liver ikihangaika katika kipindi ambacho ikiwa na mpira uwanjani ambapo mara nyingi wakicheza kwa muundo wa 4-3-3 hutumia viungo James Milner na Wijnaldum kama namba 8 (two eights) ambao sio wabinifu kiasi cha kutosha hivyo timu inakosa ubunifu. na mara nyingi katika msimu huu imeonekana Klopp akiamua kutumia muundo wa 4-2-3-1 ili kuweza kuongeza ubunifu kikosini kwa kumpanga Shedran Shaqiri (na mda mwingine Daniel Sturridge kama mshambuliaji wa mwisho), hasa katika mechi ambazo ameona atakuwa na uhakika wa umiliki wa mpira mfano mechi za EPL dhidi ya Watford, Fulham, Cardiff, Huddersfield na Southampton.

Ni mechi ambazo ilionekana fika ni kwa namna gani Liverpool iliweza kutengeneza nafasi na sio kulazimisha kama ambavyo wakicheza kwa muundo wa 4-3-3. Ingawaje ni wazi pia katika mechi hizo timu ilionekana inakosa kuwa na uwiano mzuri kwa ulinzi na ushambuliaji na kuruhusu wapinzani kujitengenezea nafasi.
Na ndivyo ambavyo naamini hii imekuwa ni changamoto kwa klopp, ni kwa jinsi gani, timu inaweza kuwa na kiasi kikubwa cha ubunifu huku ikiweza kutawala mchezo kwa wakati mmoja.

Labda ni uhtibitisho wa ile kauli maarufu iliyowahi kutolewa na Rafael Benitez kwamba “mpira ni blanketi fupi huwezi kujifunika mwili mzima” ukijifunika miguuni, kichwa kitabaki wazi na ukijifunika kichwani miuu inabaki wazi au labda falsafa za Klopp zimekuwa zikitegemea zaidi gegenpressing kuliko muunganiko wa mbinu zote (combinations) kama zilivyo timu nyingine kubwa ambazo hazina uteemezi mkubwa kwenye counter pressing bali hutumia kama njia moja wapo kati ya njia nyini za kujitenenezea nafasi.

Na ni bayana kuwa katika mpira kama unateemea zaidi mbinu moja, ni rahisi kutabirika na hivyo kuzuilika hasa unapokutana na makocha bora.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here