Home Kitaifa Ibrahim Ajibu vs Zahera Mwinyi

Ibrahim Ajibu vs Zahera Mwinyi

4749
0

Kuna wakati kocha wa Yanga Zahera Mwinyi aliwahi kumponda Ibrahim Ajibu mbele ya waandishi wa habari, watu wakalalamika sana wakidai haikuwa jambo sahihi kocha kumkosoa mchezaji hadharani wakitaka amalizane nae kimyakimya.

Baada ya muda kocha huyohuyo aliondoka nchini akaenda Congo DR kwenye majukumu ya timu yabtaifa, Yanga ikabaki chini ya Noel Mwandila alivyorudi Zahera akasema ripoti ya mahudhurio aliyopewa inaonesha Ajibu alihudhuria mazoezini siku 4 kati ya 10.

Ajibu akaanza kuchezea benchi  na Zahera akaweka msimamo wake kuwa, yupo tayari kupoteza mechi kwa kuwatumia wachezaji wanaohudhuria mazoezini kuliko kupoteza mechi akiwa amewajaza mastaa wanaokwepa mazoezi.

Juzi kati tu huyohuyo Zahera amemvua unahodha Kelvin Yondani na kumkabidhi Ajibu, show ya jana Yanga vs Mwadui kila mtu ni shahidi kwa kile alichokifanya Ajibu (alihusika katika mabao yote ya Yanga) wakati ikishinda 3-1.

Zahera amemfanya Ajibu kuwa kiongozi kwa wachezaji, ni imani kubwa sana aliyonayo juu ya Ajibu na jana baada ya Ajibu kufunga bao kwa free kick alikimbia hadi nje ya uwanja kwenda kumkumbatia kocha wake hii inatupa picha kwamba hakuna tatizo kati ya wawili hao.

Wakati Zahera anamkosoa Ajibu lengo lake lilikuwa ni kumjenga ali afanye vizuri ndio maana kwa sasa amekuwa sehemu ya kikosi cha kwanza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here