Home Uncategorized Isco anakwenda Chelsea, Rabiot kutimka PSG, Icard mshahara mdogo

Isco anakwenda Chelsea, Rabiot kutimka PSG, Icard mshahara mdogo

4003
0

Klabu ya Chelsea, ipo kwenye vita ya kumwania kiungo wa klabu ya Real Madrid, Isco. Nyota huyo pia anawaniwa n timu kama Arsenal, Manchester City, na Tottenham. Chelsea wapo tayari kutoa kitita cha paundi million 70 kumsajili kiungo huyo.Isco mwenye umri wa miaka 26 amekuwa hapati nafasi mara kwa mara ndani ya kikosi cha Real Madrid.Isco, huenda akjiunga na klabu ya Chelsea, ifikapo mwezi Januari, huku akitarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne na nusu na atakuwa anapokea mshahara wa paundi 250,000 kwa wiki.Zipo taarifa zinadai kuwa Real wamewaonya Man City kuwa Isco hauzwi chini ya Paundi Milion 100Licha ya matatizo ambayo Isco amekumbana nayo, mchezaji mwenzake Dan Cafvajal amesema Isco ana ujasiri wa kutosha wala hakatishwi tamaa na changamoto anazokutana nazo kwa sasa.


Jarida la nchini Ufaransa, limefichua kuwa kiungo wa klabu ya Paris Saint Germain Adrien Rabiot, atajiunga na klabu ya Barcelona, mwisho wa msimu huu.Rabiot, mwenye umri wa miaka 23 mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu na amegoma kusaini mkataba mpya ndani ya klabu hiyo.Hata hivyo klabu ya Barcelona, itasubiri mpaka mwisho wa msimu kumchukua kiungo huyo.


Wakala wa mshambuliaji wa Inter Mauro Icardi ambaye pia ni mke wake Bi Wanda amesema mshahara anaolipwa mume wake/mteja wake ni kiduchu mno.Wanda amesema msimu uliopita mume wake alihusishwa kujiunga na Juventus lakini hakuwa tayari. Wanda ameongeza kuwa licha ya mshahara mdogo wa Inter lakini Icardi alikataa hela nyingi za Juventus.Icardi ambaye analipwa Paundi Milioni 6 kwa mwaka amekuwa akihusishwa kuondoka klabuni hapo na anawindwa na vilabu mbalimbali kama Chelsea na Real Madrid.Yawezekana Icardi anataka fedha nyingi lakini nje ya Italia ndio sababu iliyofanya aikatae Juventus.


Dodoso: Messi ametwaa kiatu cha mchezaji mwenye magoli mengi ulaya kwa mara ya 5Lionel Messi, ametwaa tuzo ya Pichichi mara tano mfululizo.2009/10 mabao 34.2011/12 mabao 50.2012/13 mabao 46.2016/17 mabao 37.2017/18 mabao 34

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here