Home Kimataifa Jezi ya Man United yazima uhai wa mwanasoka Zimbabwe

Jezi ya Man United yazima uhai wa mwanasoka Zimbabwe

4274
0

“Alikuwa amevaa jezi ya Manchester United, nahisi walidhani ni muandamaji. Wakampiga risasi ya kichwa kisha wakamtelekeza” Maneno ya Mzee Julius Choto

“Mwanangu alikuwa tegemezi, Serikali imenipokonyoka mwanangu (huku akilia), alikuwa mwanasoka mzuri. Ndoto zake zimezimwa akiwa na miaka 22 pekee” Hii ni kauli ya baba yake Kelvin Tinashe Choto ambaye aliuwawa na polisi nchini Zimbabwe kutokana na machafuko yanayoendelea nchini humo.

Mwili wake ulikutwa siku ya pili katika kituo kidogo cha polisi mjini Harare. Choto alikuwa akijiandaa kwenda kufanya majaribio nchini Afrika kusini. Tinashe wiki iliyopita alikamilisha taratibu zote za usafiri kwenda Afrika kusini.

Tinashe alikuwa amesimama karibu na geti la polisi akinunua maembe. Polisi huyo alimshikia bunduki kichwani kwa nyuma kabla ya kumfyatulia rasasi kwa madai kuwa alikuwa amevaa tisheti nyekundu ambayo ilikuwa inavaliwa na waandamaji. Tinashe ameacha mke na mtoto mwenye umri wa miezi 7.

Machafuko yanaendelea nchini humo kutokana na vuguvugu ya kisiasa. Wapinzani wanamtaka raisi wa nchini hiyo Emmerson Mnangagwa ajiuzulu kutokana na mauaji ya kutisha yanaoendelea nchini humo. Mamia ya watu wanashikilia na polisi na idadi kubwa ya watu wameuwawa kikatili.

Walio wengi wamempa raisi huyo jina la Mamba kutokana na wingi wa watu kupoteza uhai. Raisi wa chama cha MDC Nelson Chamisa alishiriki mazishi ya Tinashe.

Tinashe hakuwa mwanasiasa, hakuwa mwanaharakati, hakuwa muandamaji lakini leo uhai wake umepotea. Ndoto zake za soka zimezima, familia imebaki na jeraha na majonzi mazito. Mwanasoka huyu angekuja kuwa tegemezi na msaada mkubwa kwa taifa.

Apumzike kwa amani Tinashe

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here