Home DOKUMENTARI Jezi ya Rashford ni nzito sana

Jezi ya Rashford ni nzito sana

15606
0

Moja ya wachezaji wakubwa kuwahi kuvaa jezi namba 10 pale Old Trafford ni Dennis Viollet, mmoja mashujaa wa Sir Matt Busby’s “Babes”

Kuna baadhi ya wachezaji waliova pia namba hizo. Mashujaa wengine ni watu kamw Sir Bobby Charlton na Duncan Edwards. Nyakati hizo Dennis Viollet alikuwa mfungaji bora wa United

Ni mchezaji wa kwanza kutokea kwenye akademi na kujiunga “Busby Babes” na alianza 1953.

Kama Charlton, Viollet nae alinusurika ajali ya Munich. Alifunga mabao 32 kwenye michezo 36 msimu wa 1959/60 na aliifungia United mabao 159 kwenye michezo 293 kabla ya kuuzwa kwa klabu ya Stoke City.

Pia yupo Stan Pearson ambaye hakujulikana sana. Stan alifunga mabao 148 kwenye michezo 343 na kuwa mfungaji bora nama 12 mabao mawili nyuma ya Ruud van Nistelrooy.

Mfumo wa Man United ulianza kubadilika baada ya 4-4-2 kuchukua nafasi kubwa. Kila mchezaji aliyecheza upande wa kushoto wa mshambuliaji wa mbele basi alipewa namba 10. Miaka ya nyuma jezi namba 10 ilikuwa na thamani kubwa Old trafford lakini baada ya mfumo huo jezi hiyo ikaanza kutumika hovyo.

Marcus Rashford nae amepewa jezi hii nzito ambayo kila mtu ataanza kumwangalia kwa jicho la kitofauti. Ni mmoja kati ya waingereza wenye bahati ya kuvaa namba hiyo. Ni Jezi nzito sana kwake. Bila shaka anahitajika kuifanyia makubwa.

Miaka ile pia alikuwepo Norman Whiteside. Mnamo 24 April 1982, kabla hajafikisha miaka 17, Norman Whiteside alikuwa mchezaji mchanga kabisa kwenye historia ya Manchester United kupata nafasi ya kikosi cha kwanza tokea Duncan Edwards alipofanya hivyo. Hata Rashford hapaswi kuogopa wala kuona kama jezi hii ni mzigo kwake kwani tayari anatembelea nyota za hapo awali. Umri sio tija wala hapaswi kukata tamaa.

Kikubwa ni jitihada na kucheza kila nafasi ambayo mwalimu atamwelekeza. Uzuri Rashford inaajulikana wazi kuwa sio kwamba ana kipaji kikubwa ila tu anajitihada. Kasi yake ni chachu kwake, hata Duncan alicheza nafasi tofauti uwanjani kama winga na fowadi. Nafasi zote hizi Rashford pia anacheza wala hakuna ugumu wowote kwake.

Inawezekana kweli jezi namba 10 ni kubwa mno Old Trafford kuliko hata jezi namba 7 ambayo baadae ilikuja kuwa ya kibiashara zaidi baada ya Cristiano Ronaldo. Zamani alikuwepo
George Best. George Best pia aliwahi kuvaa jezi namba 7. Na jezi hii namna 7 ilipata umaarufu mkubwa sana. Hata hivyo aliwahi kuvaa jezi namba 8, 10, na 11.

Alivaa jezi namba 10 mwaka 1972 ikiwa ni jezi yake ya mwisho kabla hajaondoka Old Trafford akiwa na umri wa miaka 27 tu baada ya bodi ya Manchester United na Sir Matt Busby kushindwana nae kutokana na tabia zake mbaya.

Man United ya zamani ilikuwa na kikosi kikubwa na chenye mastaa haswaa. Tunakumbuka United ya juzi wakati wa ujio wa Zlatan kumpokonya Martia jezi suala lililozua utata sana. Lakini hata united ya zamani palitokea ssintofahamu kubwa sana. United ilikuwa na Sir Bobby Charlton, George Best, na Denis Law. Hapo ushindani ulikuwa kwenye jezi namba 10 na 9. Kwa kipindi kirefu Charlton alotumika kama mshambuliaji msaidizi na mshambuliaji wa pembeni na alivaa jezi namba 8 ambayo imepoteza mvuto kwa sasa Old Trafford na 10. Katika historia ya Man United jezi namba 10 Charlton aliweka heshima kubwa na kuweka historria ya wachea 12 waliowahi kuvaa jezi hiyo mpaka kufikia Wayne Rooney katika kipindi cha miaka 60. Sasa Rashford ni mchezaji wa 13.

Marcus Rashford 18/19

Wayne Rooney (07/08 – 17/18),
Zlatan Ibrahimovic(17/18),
Ruud van Nistelrooy (01/02 – 05/06),
Teddy Sheringham (97/98 – 00/01),
David Beckham (96/97),
Roy Keane (95/96),
Mark Hughes (83/84 – 94/95),
Clayton Blackmore (90/91),
Norman Whiteside (82/83 – 87/88),
Peter Davenport (85/86 – 86/87),
Frank Stapleton (84/85 – 85/86),
Alan Brazil (84/85),
Garth Crooks (83/84),
Lou Macari (77/78),

Hata kipenzi cha waingereza David Beckham alivaa jezi namba 10 aliyoipokea kutoka kwa Mark Hughes.

Beckham alibadilishiwa jezi namba 7
Na kuchukuliwa na mtaasisi Teddy Sheringham. Katika ya wachezaji waliokuwa na akili sana uwanjani na wajanja sana. Alivaa kivuli cha Robin van Persie, alikuwa mwerevu kama Michael Carrick, alijitoa kama Rio Ferdinand, mtulivu kama Henrik Larsson, yupo makini kama Dimitar Berbatov na alikuwa na uwezo wa kukaa na mpira kama Ryan Giggs. Huyo ni Teddy Sheringham moja ya wachezaji wabunifu kuvaa jezi ya Manchester United.

Sio kama alikuwa na kasi kama Denis Bergkamp wa Arsenal, lakini alibarikiwa jicho la tatu. Alikuwa na upeo wa ajabu utadhani Iniesta. Wajerumanj hawawezi kumsahau kwa kitendo alichiwafanya Bayern Munich kwemye fainali ya Uefa. Rashford sijui kama ana uwezo wa huyu mwanaume lakini Rashford amemzid Teddy kasi kitu ambacho kinaweza kumsaidia.
Alistaafu soka katika umri wa miaka 42.
Alifunga mabao 355 kwemye michezo 898, timu ya taifa alifunga mabao 11 katika michezo 51 kwa timu taifa ya England.

Wapo waliofeli pia hivyo kama Rashford akifeli hatokuwa wa kwanza, lica ya kwamba Lou Macari alipendwa sana na mashabiki wa United baada ya kukataa ofa ya Liverpool na kujiunga na Red Devils akitokea Celtic mwaka 1973, aliifunga mabao 57 kwenye michezo 105 kwa Celtic lakini alimbwela United baada yakufunga mabao 97 ndani ya michezo 404 na mabao matano tu kwa timu yake ya taifa. Alizomewa sana uwanjani lakini aliimbwa sana uwanjani pia.

Mmoja wa mashujaa wengine ni Mark Hughes. Alisajiliwa Man United akiwa na umri wa miaka 14. Alioata mafasi akiwa na umri wa 19. Walikuwa na ushirkiano mziro sana na swahiba wake Whiteside na Frank Stapleton. Alikuwa na jezi namba 10 alifunga mabao 163 katika michezo 467 katika misimu miwili Old Trafford.

Ruud Van Nistelrooy akiwa na jezi namba 10 alifunga mabao 150 katika michezo 210 tu. Jamaa alikuwa na balaa sana huyu. Walimbatiza jina “poacher” mkali wa hatua 6 kama Chicharito.

Wayne Rooney Wazza roho ya Man United na picha halisi ya mpambanaji. Mmoja kati ya wachezaji bora kuwahi kutokea ardhi ya Uingereza. Hata golini alikuwa radhi kucheza. Akimwaga jasho na damu. Achilia mbali vurugu zake lakini ni LEGEND. Sir Alex alikuw tayari kuuza timu yote lakini sio Wazza.

Rooney alivaa namba 10 lakini mpaka anaondoka Old Trafford hakuna anayejua jamaa alikuwa anacheza namba ipi vizuri zaidi maana hata beki namba mbili msela alikaza. Rashford ana mengi ya kujifunza sana kwa Wazza kwani amewahi kumuona akiwa anacheza soka na wamecheza wote.

Denis Law alikukia Scotland. Katika maisha yake ya soka amefunga 332 katika michezo 652, ikiwa ni mabao 237 katika michezo 404 kwa upande wa Manchester United. Ni mfungaji bora namba 2 nyuma ya Sir Bobby Charlton’s mwenye mabao 249. Bobby alicheza michezo 758 kwa miaka 17 na Law alicheza miaka 11.

Law ndiye mchezaji pekee kutoka Uskochi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa ulaya (European Footballer of the Year).
Licha ya kuwa shujaa wa United laakini haawezi kusahaulika kwa goli lake aliloifunga United akiwa na klabu ya Man City bao ambalo liliishusha daraja Man United.

Makala na Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here