Home Kitaifa Kabwili anafanyiwa uchunguzi Hospitali

Kabwili anafanyiwa uchunguzi Hospitali

4031
0

Golikipa ya wa Yanga Ramadhani Kabwili bado yuko hospitali ya Selian Arusha akifanyiwa vipimo zaidi kufuatia maumivu ya nyonga aliyopata leo kwenye mechi ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya  African Lyon iliyochezwa jijini Arusha.

Kaimu Mwenyekiti wa Yanga Samwel Lukumay amesema Kabwili bado yupo hospitali madaktari wakiendelea kumfanyia uchunguzi ili kubaini ukubwa wa tatizo lake.

“Kabwili alipata matatizo kwenye nyonga na sasa hivi bado yupo chumba cha CT Scan akifanyiwa uchunguzi ili kugundua tatizo ni nini, lakini misuli ilibana na kupelekea kushindwa kabisa kuendelea na mchezo”-Samwel Lukumay, Kaimu Mwenyekiti-Yanga.

“Tunasubiri taarifa kutoka kwa daktari ili tujue anaweza kuwa nje kwa muda gani.” #GetWellSoon @_kabwili32

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here