Home Kitaifa Kaimu Rais atuliza hofu Simba

Kaimu Rais atuliza hofu Simba

9456
0

Kamati ya uchaguzi ya klabu ya Simba chini ya makamu mwenyekiti wake Stephen Ally imethibitisha kukamilika kwa zoezi la uchukuaji fomu za kugombea katika klabu hiyo huku anaekaimu nafasi ya Rais Salim Abdallah ‘Try Again akiwa hajachukua fomu.

Wadau wengi wa klabu ya Simba walikuwa wanaamini kaimu Rais wa klabu hiyo Salim Abdallah angechukua fomu ya kugombea nafasi ya urais lakini haijawa hivyo. Baadhi ya mashabiki wamekuwa na wasiwasi kwamba nani anaweza kuipa mafanikio Simba kama ilivyokuwa chini ya Try Again.

Lakini Try Again amewatoa hofu wanasimba kwa kusema bado yupo ndani ya klabu hiyo na atashirikiana kwa karibu na viongozi watakaochaguliwa kwa kuwapa ushauri na kusimamia mambo mbalimbali akiwa nje ya uongozi.

“Kwa sasa Simba haihitaji kujadili mtu, kiongozi wa Simba kwa sasa sio mtu kiongozi wa Simba ni bodi kwa maana hatatizamwa mtu mmoja kwa sababu tunazungumzia kampuni”-Salim Abdallah (kushoto pichani juu), kaimu Rais Simba SC.

“Unapozungumzia kampuni haimaanishi ni mtu fulani maana yake kampuni na mwenye kampuni ni vitu viwili tofauti kwa hiyo niwatoe hofu wanasimba kwamba wasiwe na wasiwasi Simba iko salama na imara na mimi kama mwanachama mkereketwa nitaendelea kubaki kiongozi kwa kushauri na kuonesha njia kwa uzoefu wangu nilioupata kidogo kuhakikisha Simba inaendelea kufanya vizuri.”

“Muundo wa Simba wa sasa sio wa kuongozwa na mtu mmoja kama ilivyo sasa tunazungumzia kampuni yenye bodi ya wakurugenzi wahasibu ma-CEO kwa hiyo hao wote wataendelea kuiongoza Simba kwa ufanisi. Nina hakika tutafanikiwa kwa sababu na sisi tupo kwa ajili ya kushauri na kusimamia.”

“Niwahakikishie wanamsimbazi kwamba wasiwe na wasiwasi, tulikaa tulitulia tukatengeneza na hatimaye tumefikia hapo, kutokugombea kwangu hakumaanishi kwamba Simba inarudi nyuma. Simba inakwenda mbele na itaendelea kufanya vizuri kadiri siku zinavyokwenda.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here