Home Kitaifa Kambi ya Zanzibar kujaribu kusimamisha unyonge wa Prisons kwa Simba

Kambi ya Zanzibar kujaribu kusimamisha unyonge wa Prisons kwa Simba

9510
0

Kikosi cha maafande wa Prisons kutoka jijini Mbeya kimetua hii leo jiji Dar Es Laam wakitokea visiwani Zanzibar ambako waliweka kambi maalum kwa ajili ya kumuua mnyama Simba hapo kesho.Kuonesha namna ambavyo wamepania kuisimamisha Simba, klabu hiyo ya Mbeya hawakupumzika na walikwenda moja kwa moja uwanja wa Taifa kwa mazoezi ya mwisho kujiandaa na mchezo huo.Lakini Prisons itawabidi kuingia kwa tahadhari kubwa sana katika mchezo wa kesho sio tu kutokana na ubora wa Simba msimu huu lakini pia rekodi yao mbovu mbele ya Mnyama.Katika mechi 5 zilizopita kati ya Simba na Prisons maafande hao walifanikiwa kupata ushindi katika mechi moja tu, ambapo mchezo huo ulikuwa wa November 16 pale mjini Mbeya, Simba akafa 2-1.Lakini michezo yote iliyobaki Simba walishinda huku msimu uliopita wakiwapiga mara mbili, na mara ya mwisho ilikuwa taifa Simba akishinda 2-0 kwa mabao ya John Boko na Emmanuel Okwi.Kwa upande wa Simba sasa hawana hofu kwani dakatari wa timu hiyo amesema kuna uwezekano 75%+ Okwi akawepo uwanjani hapo kesho baada ya kuumia katika mchezo wa ngao ya hisani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here