Home Kimataifa Kane atokwa na povu, Seedorf aponea chupuchupu

Kane atokwa na povu, Seedorf aponea chupuchupu

10345
0

Baada ya Englad kufungwa mabao 2 kwa 1 na Hispania katika uwanja wao wa nyumbanj nahodha wa England amemtupia lawama refa wa mchezo huo.

Harry Kane amesema Danny Welbeck hakumchezea faulo De Gea. Kane anasema Welbeck akikuwa amesimama na De gea aliruka juu mwenyewe akadondoka na kuupoteza mpira na hukukuwa na faulo yoyote

Hata hivyo nahodha huyo amesifu kikosi chake na kusema kuwa walicheza vizuri kulingana na maelekezo ya mwalimu.

Amekiri kuwa yapo matatizo ya hapa na pale lakini anamlaumu mwamuzi kwakuwa ndiye aliyefanya wao kupoteza mchezo huo.

Amesema refa huyo alizidiwa kabisa katika mchezo huo na akishindwa kwenda na kasi ya mchezo huo.

Amesema kama mwamuzi angekuwa ametulia na kujiamini basi bao la kusawazisha na England halikuwa na tatizo lolote.

Hii ni kwa mara yao ya kwanza England kufungwa mara tatu mfululizo tokea mwaka 1988. England walifungwa na Croatia, Belgium katika kombe la dunia kabla ya kichapo cha nyumbani kutoka kwa wahispaniaola.

Kipigo cha jana ni cha pili tokea mwaka 2007 kufungwa ardhi ya ya nyumbani. Croatia walifanya hivyo mara ya mwisho 2007.

Harry Kane pia alionesha kiatu chake cha mfungaji bora wa Kombe la dunia kwa mara ya kwanza mbele ya mashabiki.


Seedorf aponea chupuchupu

Nguli wa soka wa zamani Clarence Seedorf jana amefanikiwa kupata sare yake katika mchezo wake wa kwanza akiwa na timu ya taifa ya Cameroon, walipocheza na timu dhaifu kabisa kutoka visiwa vya Comoro.

El Fardou Ben Mohamed nyota kutoka Red Star Belgrade aliwapa uongozi Comoro wanaoshikilia nafasi ya 102 ya fifa mbele ya mabingwa wa Cup of Nations

Ilichukua takribani dakika 65 ndipo Indomitable Lions kupata bao la kusawazisha kupitia mchezaji alaikichapa ligi kuu Ufaransa Stephane Bahoken, na kumpa matumaini nyota huyu wa zamani Real Madrid alama moja kwenye mchezo wake wa kwanza kama kocha wa timu hiyo ya taifa.

Seedorf, ambaye kocha wake msaidizi pia ni mdachi mwenzie Patrick Kluivert, waliwahi kufanya kazi pamoja kwa muda wa miezi 6 katika vilabu vya AC Milan na Deportivo la Coruna.

Cameroon walifuzu moja kwa moja michuano ya 2019 kama muandaani lakini wanacheza na timu za group B.


Kwingineko Mo Salah na timu yake ya taifa wametoa dozi ya mabao 6 kwa 0 kwa Niger huku Salah akifunga mabao matatu

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here