Home Kitaifa Katibu Coastal Union ang’atuka

Katibu Coastal Union ang’atuka

4271
0

Katibu Mkuu wa Coastal Union Abdulatif Omary Samau ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya ukatibu baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miezi mitatu.

“Ni kweli nimejiuzulu kutoka kuwa katibu mkuu wa Coastal Union, nitabaki kuwa mwanachama wa kawaida. Nimehudumu tangu mwezi wa 9 mwanzoni mpaka mwishoni mwa mwezi wa 12 kwa hiyo nimeona niweke wazi kujiuzulu kwangu kwa sababu kwa siku napokea zaidi ya simu 10.

“Niliajiriwa kwa mkataba wa mwaka mmoja na niliwapa notice ya mwezi mmoja kabla (mwezi wa 12 mwanzoni) kwa kuwaandikia barua kuwa najiuzulu nafasi yangu ili watafute mtu mwingine ikifika December 31 nitakuwa si katibu tena wa Coastal Union.”

“Sababu zipo nyingi lakini kuna sababu moja kubwa, wakati naajiriwa Coastal Union nilikuwa nina shughuli zangu binafsi kama kijana, ikabidi niweke pambeni shughuli zangu ili nifanye shughuli za Coastal lakini sasa nimeona nirudi kwenye shughuli zangu kwa sababu zina dorora na waswahili wanasema mshika mawili moja humponyoka.”

Inasemekana viongozi hawazungumzi lugha moja ndani ya kamati ya utendaji na baadhi wamejigawa, kuna kundi la uongozi la Dar na kundi jingine la Tanga.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here