Home Kimataifa Kichaa Biesla anatisha kama ukoma

Kichaa Biesla anatisha kama ukoma

5485
0

Jina la Leeds United sio geni sana miongoni kwa wafuatiliaji wa soka la nchini Uingereza, ni timu iliyokuwa na mafanikio makubwa mwanzoni kwa miaka ya 2000. Mafanikio yao kwa kiasi kikubwa yalichagizwa na ubora wa wachezaji walikuwa nao pamoja na muunganiko mzuri (mbinu).

Wachezaji kama Rio Ferdinand, Jonathan Woodgate, Lucas Radebe, Robbie Keane, Mark Viduka, Harry Kewell na Alan Smith walipata kuunganishwa vizuri na kocha David O’Leary na kufanya Leeds kucheza soka la kuvutia na kufika Hadi hatua ya Nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya ambapo hatimaye walitolewa na Valencia iliyokuwa katika kiwango bora wakati huo.

Miaka michache baadae Leeds ilipata changamoto za kiuchumi na kiutawala na kusababisha kuuzwa kwa wachezaji wengi bora na kisha timu ikashuka daraja na yangu hapo haijafanikiwa kupata tena. Na zaidi hakukuwa na dalili za kupanda daraja mpaka mwezi Juni mwaka 2018. Leeds walionekana kuwa makini zaidi na swala hilo kwani walimleta kocha Marcelo Biesla ambaye ni moja kati ya makocha wenye uwezo mkubwa wa kufundisha soka.

Mbinu zake za kushambulia kwa kasi bila woga zimempatia jina la “IL LOCCO” ikiwa na maana ya kichaa. Na hawakukosea sana kwani Biesla ni kichaa wa mbinu na ubinifu. Makocha kama Pep Guardiola, Diego Simeone na Maurizio Pochetino wamekiri katika nyakati tofauti kuwa wanamkubali Biesla na kuiga mbinu zake.

Guardiola alishawahi kusema kuwa “Biesla ndie KOCHA bora zaidi duniani” wakati huo Biesla akifundisha Athletic Bilbao ya kina Ander Herrera, Ikar Munian, Fernando Llorente na Javier Martinez huku Guardiola akiwa Barcelona. Mechi zilizowakutanisha, zilikuwa za kuvutia sana kwa wapenda mbinu. Biesla ameichukua Leeds na kuibadilisha kwa kiasi kikubwa, sio kwa kusajili wtu wenye uwezo mkubwa Bali ni kwa kuwekeza katika mbinu na kuwatengeneza wachezaji waendane na mbinu hizo.

Hadi sasa zikiwa zimechezwa mech 24 tayari Leeds inaongoza ligi (championship) ukiwa na jumla ya alama 51 na ikiwa imetokea kushinda mechi 7 mfululizo zikiwemo zote walizocheza katika kipindi cha sikukuu mwezi wa 12 ambao ni mwezi wenye mechi nyingi mfululizo.

Biesla hupendelea sana mfumo wa 3-3-1-3 na Mara nyingi hata kama hupadilisha muundo wa wachezaj uwanjani lakini dhana hubaki kuwa ile ile, na ndivyo alivyoifanya Leeds msimu huu katika championship ambapo licha ya mfumo wa 4-1-4-1 na 4-2-3-1 ambapo wamekuwa wakiutumia. Mmabeki wa pembeni huingia ndani kushambulia kisha kutafuta pembe tatu na kupiga pasi na kumfikia kiungo mshambuliaji ambaye waargentina wanamwita “Enganche”.

Kisha baada ya kupokea mpira katika eneo hilo la uwazi, Biesla huwataka washambuliaji wake wa pembeni kutoa mapana, huku mshambuliaji wa kati mbele kuwa katikati na hiyo kumrahisishia “Engache” kazi kwa kupiga Pasi ya mwisho. Katika nafasi hii Biesla amemfanya Pablo Hernandez kuwa moto ambapo hadi sasa ametoa Pasi 10 za magoli katika Championship msimu huu.

Sambamba na hilo Leeds ina miliki mpira kwa sehemu kubwa ya michezo inayocheza, ukiwa na wastani wa zaidi ya 63% ya umiliki wa mpira kwa mechi (asilimia 5 zaidi yatimu yoyote katika mashindano hayo).
UUmiliki wa mpira unawafanya Leeds kuwa na mda mwingi wa kuamua nini wafanye wa Napoli wa na mpira na kwa uzuri tumeweza kuona Yale yaliyoandikwa na kocha Jed C.

Davies kwenye kitabu cha “THE PHILOSOPHY OF FOOTBALL: IN THE SHADOWS OF MARCELO BIESLA” ametulezea namna tatu za utengenezaji wa nafasi kwa Marcelo Biesla ambazo ni kutanua uwanja (mapana), Kuwavuta wapinzani kaajili ya kupata nafasi kati ya mistari ya wachezaji (between the lines) na pia kujaza watu upande mmoja na kisha kuhamisha upande wa ushambuliaji kwa haraka.

Haya yote yameonekana katika Leeds ya Marcelo Biesla. Vile vile katika kushambulia Biesla anaamini eneo ya mbele ya goli la upanzani likijulikana kama eneo la dhahabu au pembe C kwa baadhi ya makocha ambalo huzalisha zaidi ya 80% ya magoli yote yanayofungwa, ndio eneo linalofaha kushambuliwa zaidi. Mshambuliaji Kemar Roofe akiwa katika kiwango bora kabisa amefunga jumla ya magoli 13 na hayo yote ameyafunga ndani ya boksi katika eneo hilo.

Katika kuzuia, Leeds unaonekana kuzuia kama timu ambapo timu yoote hukaba kuanzia juu katika Muunganiko sahihi, ikijaribu kuupora mpira kwa haraka kutoka kwa wapinzani na kuuweka katika himaya yap kisha kutekeleza Yale ambayo KOCHA ameyakusudia kuyafanya timu inapokuwa na mpira, Leeds imefungwa magoli 22 katika mechi 24 za championship msimu huu wakiwa na jumla ya Clean sheet 10.

Mzunguko wa pili ukiwa umeanza, Leeds wanaonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kurudi katika Ligi kuu ya uingereza na kuendelea kunogesha soka la uingereza kwani tutapata kushuhudia makocha wazuri na wabunifu wakikabiliana na hiyo kutoa burudani ya uhakika.


Makala na Robert Komba
0762283468, Robbiekomba@gmail.com

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here