Home Uncategorized Kinaiporomosha Man United ya Mourinho

Kinaiporomosha Man United ya Mourinho

6585
0

Na Robert Komba
Manchester united klabu yenye mashabiki wengi zaidi duniani kutokana na takwimu za hivi karibuni, ipo katika hali isiyowalidhisha mashabiki wake wengi ulimwenguni kote. Wamekuwa na kiwango cha kawaida hasa katika ligi na wadau wa soka wamejaribu kutoa maoni yao ni kwanini timu hiyo haifanyi kile kinachotarajiwa, na zaidi kuna baadhi wamechukua hatua ya kumlaumu kocha Jose Mourinho kwa mambo kadhaa yanayotokea. Hivi ndivyo ambavyo mimi naweza kuielezea hali ya klabu hiyo:
KIMBINU: HAWATUMII PRESSING KAMA NJIA YA KUTENGENEZA NAFASI ZA MAGOLI BALI NJIA YA KUJILINDA

Katika ulimwengu wa sasa pressing imeutawala mpira, kila timu inatumia mbinu hii katika nadharia yake ya kiufundi na hasa ni ule mkazo wa eneo la juu ya uwanja (counter pressing) lengo likiwa kwanza ni kuwazuia wapinzani wasiweze kutengeneza mashambulizi yao vizuri, lakini pia kujaribu kupata mpira karibu na goli la wapinzani na hivyo kuwa na pasi chache kabla ya goli kama anavyoeleza kocha wa Liverpool;

Jurgen Klopp kwamba hakuna mchezaji aliyekuwa fundi anayeweza kutengeneza nafasi kuliko counter pressing au kama inavyofahamika kijerumani eenpressing. Katika lii ya uingereza hadi sasa timu zote ambazo ziko katika 7 bora kwenye msimamo zipo pia katika timu kumi zinaongoza kwa kuchukua mipira kwenye eneo la juu ya uwanja (final third) isipokuwa kwa Manchester united ambayo ni ya 19 katika takwimu za timu zinazokabia juu ikiwa imepokonya mpira mara 31 tu katika mechi 13, hii inaonyesha fika ya kuwa Manchester united inajipunguzia nafasi ya kujitengenezea nafasi za kupata magoli, na haishangazi kuona kwamba hawajafunga magoli mengi hadi sasa.

UFINYU WA NAFASI KWA ROMERO LUKAKU
Romero Lukaku ndio amekuwa mbuzi wa kafara kwa upande wa wachezaji na wengi wanamlaumu Mourinho kwa kutomweka benchi, ijapokuwa wengi wameshindwa kujibu swali la msingi kwanini Lukaku amekuwa na mwenendo mzuri katika timu ya taifa? Jibu la wazi kwa swali hili ni idadi ya nafasi anazopata, Lukaku amepata nafasi ya kupiga mashuti 10 tu yaliyolenga lango hadi sasa na manne kati ya hayo amefunga na amekosa nafasi kubwa 5 tu za magoli.

Ukilinganisha na washambuliaji kama Harry Kane Wilson na Mohamed Salah ambao wameonekana kuwa na form nzuri wote wamepata nafasi ya kupiga mashuti zaidi na kukosa zaidi ya Lukaku.

Kitu ambacho wengi hawakiongei ni kuwa ni kawaida kwa washambuliaji kukosa magoli, ila muhimu ni idadi ya nafasi anazotengenezewa mshambuliaji ili apate kujaribu zaidi na zaidi.

Pia takwimu za viungo washambuliaji na mabeki wa pembeni wa Manchester united ni ushuhuda kwamba Lukaku hapati nafasi za kutosha kwani katika wachezaji 20 wanaoongoza kwa kupiga pasi zilizopelekea mashuti (key passes) hakuna hata mmoja wa Man united

Hivyo ni busara kuhitimisha kuwa Mnchester united inatumia mbinu nyini kati ya mbinu za kisasa zinazotumiwa na timu nyingine kubwa, lakini katika kiasi kidogo. Na katika muktadha wa ligi iliyosheheni makocha wenye ufundi mbalimbali kama EPL Mourinho anapata anachostahili.s

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here