Home Kitaifa Kioo cha Kakolanya sio sahihi kujitazama

Kioo cha Kakolanya sio sahihi kujitazama

5302
0

Kuachilia mbali matokeo ya kushangaza yanga inayopata kutokana na maandalizi
kabla ya msimu pamoja na hali ya kiuchumi Yanga inayopitia hivi sasa.


Jina la kipa wao nambari moja na namba mbili kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania
Taifa stars Beno David Kakolanya limekuwa katika minong’ono mikubwa na kusemwa
Sana midomoni mwa mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu hapa nchini, hii
Inatokana na kile kinachodaiwa Beno kugomea mazoezi na kujiunga na wanajangwani toka alipotoka kwenye majukumu ya timu ya taifa.

Pili akihusishwa kwenda kwenye
moja ya club kubwa hapa nchini. Beno anadai ameamua kutokujiunga na kutohudhuri mazoezi ya wanajangwani kutokana na kile kutokuwa sawa na waajiri wake kimasilahi ambapo ni zaidi ya miezi minne hajapatiwa mshahara wake, kisheria pindi mwajiri anaposhindwa kulipa sitahiki za mwajiliwa wake kwa kipindi cha miezi minne ni dhahiri kuwa timu inakuwa imevunja mkataba na mchezaji wake yenyewe, kivuli ambacho Beno
anakitumia kujihifadhi, hivyo Beno yaweza kuwa anasimamia msimamo wake katika hilo.

Lakini pamoja na hayo Beno ni kijana mdogo sana mwenye kipaji kikubwa hasa pale
anaposimama kwenye milingoti mitatu, kwa hiyo anahitaji mda mwingi ili aweze
kuboresha kiwango chake.

Kwa mtazamo wa kawaida na hasi unaweza fikiri Beno yuko sahihi kutokana na ili
Binadamu aishi anahitaji mahitaji kama mavazi, malazi na chakula ambayo yote kwa
Pamoja yanakamilishwa kwa uwepo wa uwezeshwaji wa kifedha ambao Beno
Anavikosa kwa sasa hapo mitaa ya jangwani, kitu pekee ambacho Beno anatakiwa kujua,
mpira ni ajira yake hivyo anatakiwa kuuheshimu na kuupa kipaumbele katika maisha yake.

Kimsingi Beno anatakiwa atumikie club yake na mambo ya sheria ayafate pale anapokuwa
ametimiza wajibu wake wa kucheza, huku maswala ya kisheria awaachie wenye mamlaka nayo, kwani sheria ipo kutekeleza haki.

Mpaka sasa kwa yale afanyayo Beno wanayaona vijana wengi ambao wao wanamwangalia yeye kama icon wao kwenye mpira wa miguu hivyo siomtu sahihi wa kumuiga, na vijana wanatakiwa kutambua kwa yale afanyayo sio kioo sahihi
Kwa wao kujitazama taswira zao kupitia Beno mpaka pale atakapobadilika.

“KIOO CHA KAKOLANYA SIO SAHIHI KWA WACHEZAJI KUJITAZAMA”
Raphael Lucas (UDOM).
0710690782/0764764449

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here