Home Kimataifa Kipi kimemfanya Modric kuwa bora msimu uliopita?

Kipi kimemfanya Modric kuwa bora msimu uliopita?

4583
0

Luka Modric, ni moja ya wachezaji wenye nidhamu ya hali ya juu akiwa uwanjani kiukweli amekuwa anajituma sana wakati anatoka klabu ya Tottenham, na kujiunga na klabu ya Real Madrid, hakuna mtu alikuwa anategemea kama angepata nafasi ya kuanza katika kikosi hicho cha Real Madrid, kilichojaa mafundi katika eneo la kiungo kujituma kwake ndo kumemfanya Luka Modric,leo hii apate mafanikio.

Modric alijiunga na klabu ya Real Madrid msimu wa mwaka 2012 kwa ada ya uhamisho wa paundi million 45 wengi walijiuliza ataweza kufiti Real Madrid, na sio kama alitoka Tottenham, akiwa mchezaji wa kawaida hapana ila alikutana na baadhi ya wachezaji katika eneo hilo la viungo wachezaji ni Khedira Alonso, Diarra, na Ozil,katika mafanikio uvumilvu lazima leo hii wale viungo walikuwa wana mnyima usingizi Modric ,wapo wengi?wengine wasistafuu wengi wapo timu zengine.

Katika maisha ni uvumilivu Modric, ametufundisha nini katika maisha ni kujituma na uvumilivu zaidi ndani ya kikosi cha Real Madrid, amekuwa ni mchezaji muhimu sana wachache watakaoweza kugundua mchango wake kutokana na eneo analo cheza kiungo huyo.

Mimi huwa naamini katika mchezo wa soka eneo la kiungo ndo sehemu muhimu zaidi kwa sababu muda mwingi ndo wachezaji wanaofanya ulinzi na hata kupika mabao na kupeleka mipira kwa washambuliaji ili wafungee mabao.

Modric, amekuwa ni mchezaji mwenye nidhamu na ni mtakatifu hii safari ya tuzo ilianzia kwenye kombe la dunia alionyesha kiwango bora japo nchi au taifa alikuwa anacheza ni ndogo lakini amejituma na kuwafukisha fainali kwa mara ya kwanza katika historia yao.

Wapo watakosea ana umuhimu katika eneo analocheza imekuwa ngumu au aijazoeleka sana mchezaji anayecheza idara hiyo kutwaa tuzo hiyo .

Pengine me naweza kusema huu ulikuwa mwaka wake katika maisha yake hatokuja kusahau ndani ya mwaka huu ametoa kombe la Uefa, ametwaa mchezaji bora wa michuano ya Uefa, tuzo ya mchezaji bora wa fainali za kombe la dunia kiukweli alistahili sana.

Wapo watakosema labda Ronaldo,alistahili kwa sababu kila msimu alikuwa anafunga bao 40-50 na kuendelea je hayo mabao yanatokea sehemu gani katika idara ya kiungo ndo muhimili wa timu kwa asilimia kubwa kama kiungo anaweza kutengeneza nafasi za mabao basi katika timu yoyote anaweza kufunga bao au mabao.

Modric, katufundisha pia katika maisha kujituma ni kitu muhimu sana tusichoke nafikiri sasa Modric ,kwa mafanikio aliyopata na umri wake ni muda wa kutuaga na kumpizika kuna kitu gani kakosa katika ngazi ya klabu?

Licha ya kupoteza fainali ya kombe la dunia kufika fainali ni moja ya mafanikio katika nchini ya Croatia, mara ya mwisho kufika hatua kubwa ilikuwa mwaka 1998 fainali za wenyeji Ufaransa, waliiishia hatua ya nusu fainali ila sio kizazi hichi ni kizazi cha kina Slaven Billic,Anthony Seric.

By Azizi Mtambo 15

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here