Home Kitaifa KISA yamaliza utata wa Gustapha Saimon wa Yanga

KISA yamaliza utata wa Gustapha Saimon wa Yanga

4142
0

Mohammed Chiwanga Mkurugenzi wa kituo cha KISA ambapo mchezaji Gustapha Saimon alikuwa akilelewa amesema, mchezaji huyo anatumiwa kihalali na Yanga na taratibu zote zilifuatwa.

Klabu ya Dar City ya ligi daraja la kwanza Tanzania bara pia inadai mchezaji huyo ni wao na anamkataba hadi mwezi Julai mwaka huu.

“Dar City walikuwa kumuomba mchezaji (Gustapha) 2017 walikuwa wanakwenda kucheza ligi ya mabingwa wa mikoa. Tukafata utaratibu rasmi wa kumpeleka Gustapha Dar City kwa mkopo mashindano ya ligi ya mabingwa lakini baada ya mashindanonalitakiwa arudi kituoni.”

“Lakini Dar Citu baada ya usajili wa msimu huu walivyoandika nilipeleka pingamizi TFF na kupitia kamati ya haki na hadhi za wachezaji walikubali kuliondoa jina la Gustapha Saimon kutoka Dar City na kutumika Yanga.”

“Kutokana na mkanganyiko wao, wakaitoa leseni kwenda Dar City lakini mwishoni kamati ilikaa tena ikaifuta leseni ya Dar City na kumtambua Gustapha Saimon ni mchezaji wa Yanga.”

“Yanga wamefuata utaratibu na kupata ridhaa ya kituo cha KISA, wamepata barua, mkataba, kwa hiyo wao ndio wamiliki halali wa mchezaji.”

Afisa habari wa TFF Clifford Ndimbo amethibitisha kuwepo na malalamiko rasmi kutoka Singida United wakiilalamikia Yanga kumtumia Gustapha Saimon kwenye mchezo wao wa ligi wakidai ni mchezaji wa Dar City.

“Ni kweli kwamba Singida United wamewasilisha malalamiko yao kuhusiana na mchezaji huyo na vitu hiyo vinafanyiwa kazi, pale vitakapokuwa tayari tutawaambia nini kimeendelea lakini malalamiko ni kweli yameshawasilishwa.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here