Home VPL Klabu mpya ya Hassan Kessy, Usipime! Simba na Yanga zinasubiri

Klabu mpya ya Hassan Kessy, Usipime! Simba na Yanga zinasubiri

16006
0

Hivi karibuni Hassan Kessy amejiunga na klabu ya Nkana Fc ya Zambia na kukabidhiwa jezi nambari 22.

Nkana Fc ni timu gani?

Kichapo chao cha mwisho kutoka kwa Tunisia kiliwanyima nafasi Zambia ya kushirii kombe la dunia mwaka 1990. Mwaka huo huo Nkana Red Devils walifika fainali ya klabu bingwa Afrika. Hakika walikuwa na kizazi hatari zaidi.

Ukipita kule Kitwe ukitaja jina “Kalampa”, ovyo ovyo unaweza kujikuta sero. Kalampa lilikuwa jina maarufu sana kwa mashetani hawa wekundu wa Zambia. Ililuwa chini ya mwalimu Moses Simwala, chini ya mafundi wa mzee Malitoli ndugu hawa wawili (Kenneth na Mordon), kule Reuben maarufu kama “Kamanga” Sakala, marehemu mzee Kapambwe alijulikana sana kama “Gentile” Mulenga, pia alikiwepo mheshimiwa Golden Kazika mtu hatari sana nyakati zake, alikuwepo Godfrey Muselepete, Gibby Mbasela na mtaalam Beston Chambeshi. Kikosi hiki kimebeba mataji mengi zaidi katika hitsoria ya Zambia (Zambian Super League) vikombe 11 kutokea miaka 1980/90s.

Mafanikio yake ilifanya uwanja wa Nkana Stadium kujulikana huko kwao kama Mecca ya soka. Ilikuwa moja ya vilabu vitanovikubwa sana zaidi katika bara la Afrika miaka 1990. Licha ya kupoteza ubingwa kwa Power Rangers 1990, mwaka uliofuata walitwaa ubingwa wa African Cup-Winners’ Cup. Tokea miaka ya 1980 palikiwepo na uwezekaji mkubwa sana kwenye soka lao. Raisi wa Zambia wakati ule Kenneth Kaunda alikuwa anapenda soka kama Mourinho anavyopenda kupaki mabasi. Kaunda ulikuwa humwambii kitu kuhusu soka. Kaunda aliiongoza Zambia kwa miaka 27. Miaka ya 1980s mambo yakenda kwao mrama hasa kiuchumi kitendo kilichowafanya wao kujiondoa kwenye kuandaa michuano ya Afrika mwaka 1988.

Nkana FC ni moja ya vilabu vikongwa zaidi katika taifa la Zambia iliyoanzishwa mwaka 1935 katika viunga vya Kitwe mjini Wusakili . Hapo awali klabu hii ilijulikana kama Rhokana United FC kabla ya kubadilishwa na kuitwa Nkana Red Devils. Mnamo mwaka 1990 klabu hii ilifanya makubwa baada ya kufika fainali ya klabu bingwa barani afrika.

Klabu hii ya Nkana imeshindwa ubingwa wa Zambia mara 12 na mara yao ya mwisho ikiwa mwaka 2013.

Mwezi mei 23 2014, klabu hii ilipigwa na msiba mkubwa baafa ya aliyekuwa mkufunzi wake Masautso Mwale kufariki kwenye ajali ya barabarani akiwa anaelekea kwenye mchezo wao dhidi ya Séwé Sport kutoka Ivory Coast kwemye mchezo wa kundi B la CAF Confederation Cup.

Moja ya michezo migumu ya Zambia ni mchezo wa Nkana Fc vs Power Dynamos F.C ambapo mchezo huu unajulikana kama dabi ya Kopala.

Mafanaikio

Klabu bingwa(African Cup of Champions Clubs)
Mshindi wa pili: 1: 1990

Ubingwa wa ligi kuu Zambia (Zambian Premier League): 12:
1982, 1983, 1985, 1986, 1988, 1989, 1990, 1992, 1993, 1999, 2001, 2013Zambian Cup: 61986, 1989, 1991, 1992, 1993, 2000

Kombe la Chalenji (Zambian Challenge Cup): 7:
1964, 1966 (as Rhokana United)1992, 1993, 1998, 1999, 2000

Ubingwa wa Mabingwa (Zambian Champion of Champions Cup): 2:
1986, 1993

Ngao ya Jamii (Zambian Charity Shield): 13:
1982, 1983, 1984, 1985, 1987, 1989, 1990, 1991, 1993, 1994, 1995, 2000, 2014

Ushiriki wao wa michuano ya CAF

Klabu bingwa CAF Champions League: 3 walishiriki
2000 – Mzunguko wa pili
2002 – Mzunguko wa pili
2014 – Mzunguko wa pili

Hapo awali
African Cup of Champions Clubs: 9 walishiriki

1983: Nusu-fainali
1984: Robo-fainali
1986: Nusu-fainali
1987: Mzunguko wa pili
1989: Nusu-fainali
1990: Fainali
1991: Nusu-fainali
1992: Robo-fainali
1993: Robo-fainali

Washindi wa CAF (CAF Cup Winners’ Cup): 2
walishiriki
1998 – Robo-fainali
2001 – Mzunguko wa pili

CAF Cup: 1
1999 – Mzunguko wa pili

Na Privaldinho

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here