Home Ligi EPL Klopp dokta mwenye gundu, anayejaribu kutibu mikosi ya Liver

Klopp dokta mwenye gundu, anayejaribu kutibu mikosi ya Liver

5303
0

Liverpool mabingwa wa kufeli. Samahani kwa lugha isiyo rafiki kwao. Mara kadhaa Liverpool wamekuwa na msimu mzuri lakini mzimu wa kushindwa kumaliza mbio salama umekuwa ukiwasumbua sana.

Mbaya zaidi Liverpool ya sasa ina kocha ambaye mara kadhaa nae amekuwa na nyota ya kipinzani miaka yote. Klopp amekuwa na bahati mbaya sana katika kumalizia furaha ya mashabiki wake. Msimu huu tukiachilia mbali rekodi mbaya za Klopp lakini kuna mengi ya kukumbukwa ya Liverpool ambayo sio hadithi njema kwao

Kwa kipindi kirefu liverpool wameishi kwenye kiu ya mataji ya EPL. Kiu yao imeambatana na misimu mibovu na yenye mikosi na misikusuko ya kila aina.

Takwimu za Liverpool tokea mara yao ya mwisho kutwaa ubingwa 1989.

Msimu M W S L GF GA GD Pts No
1988 40 26 12 2 87 24 63 90 1
1989 38 22 10 6 65 28 37 76 2
1990 38 23 10 5 78 37 41 79 1
1991 38 23 7 8 77 40 37 76 2
1992 42 16 16 10 47 40 7 64 6
1993 42 16 11 15 62 55 7 59 6
1994 42 17 9 16 59 55 4 60 8
1995 42 21 11 10 65 37 28 74 4
1996 38 20 11 7 70 34 36 71 3
1997 38 19 11 8 62 37 25 68 4
1998 38 18 11 9 68 42 26 65 3
1999 38 15 9 14 68 49 19 54 7
2000 38 19 10 9 51 30 21 67 4
2001 38 20 9 9 71 39 32 69 3
2002 38 24 8 6 67 30 37 80 2

Baada ya kutwaa ubingwa 1989 walicheza misimu 10 bila kumaliza nafasi 2 za juu. Lakini mzimu wao ukawatafuna mwaka 2002 tena, ambapo waliongoza ligi mpaka kufikia Disemba wakiwa alama 11 mbele ya Man United.


Kwa haraka haraka msimu huu Liverpool wamepata alama moja dhidi ya Chelsea kupitia kombora la Daniel Sturridge, halafu mtoto wa mkimbizi Xedan Shakiri akapeleka kilio na simanzi kubwa kwa familia ya Jose Mourinho.


Msimu wa 2002 ambao Liverpool ilijaribu kutwaa ubingwa kabla ya kutoka kuongoza kwa alama 11 mbele ya United kabla hawajashuka mpaka mpaka nafasi ya 5 nyuma ya United kwa alama 5.

Kama Liverpool alivyopata matokeo kwa Arsenal na United msimuu, msimu wa 2002 Ilipofika januari Liverpool walisafiri mpaka Highbury na Old Trafford. Liverpool kupitia Danny Murphy aliwapa Merseyside alama 3 kutoka kwa United, kisha John Arne Riise akawahakikishia alama moja kutoka kwa Arsenal, na kuipa Manchester United uongozi kwa mara ya kwanza kwenye ligi. Msimu huo Liverpool wakamaliza nafasi ya 2 kwenye ligi.


Ilipita tena miaka 6 ndipo Liverpool msimu wa 2008-09 wakafufua tena matumaini ya kunyakua ubingwa wa ligi kuu kwa mara yao ya kwanza.


Ni msimu ambayo walimsajili Fernando Tores. Tores msimu ule alifunga magoli 33. Msimu ule Liver walimaliza wakiwa na rekodi nzuri ya kufungwa mechi chache tu. Walifunga mechi 2 msimu mzima  wakamaliza wa pili nyuma ya United kwa alama moja tu.

Ilikuwa Liverpool iliyotisha haswa. Mzunguko wa kwanza walifungwa mechi 1 tu ambao ulikuwa dhidi ya Spurs bao 2 kwa 1. Ni ile Liverpool ambayo ilimtungua Fergie pale pale OT magoli manne kwa moja. Msimu huo waliweka rekodi ya kufungwa mechi chache zaidi mechi (2) ambayo iliwekwa mwaka 1989.

Licha ya kushinda mechi 24, kutoka sare 12 mechi na kufungwa mechi 2 pekee haikutosha wao kupata ubingwa. Waliongoza ligi kwa takribani mechi 7 kutoka novemba mpaka januari lakini sare 2 kutoka kwa Wigan, Man City na kichapo kutoka kwa Middlesborough iliwaondoa kwenye uongozi na kwenda hadi nafasi ya 3. Baadae walijikongoja na kurudi nafasi ya pili lakini Fergie hakuruhusu kuacha upenyo wa kupoteza ubingwa.

Msimu wa 2013-14 Liverpool waliweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kumaliza nafasi ya pili ikiwa na idadi kubwa ya mabao ya kufunga magoli 101 na kiweka rekodi ya kuwa timu ya tatu katika historia ya ligi kufunga magoli mengi kwa msimu. Hiyo ndiyo ilikuwa Liverpool ya Suarez.

Suarez alimaliza msimu na magoli 31, Gerrard akamaliza na assists 13. Ilipofika mechi ya 32 Liverpool walimbutua Tottenham goli 4-0, wakawatwangwa Man City 3-2, Norwich 3-2, kisha wakiwa nyumbani wakawakaribisha Chelsea. Mchezo huo Gerrard akatoa boko Liverpool wakapogwa 2-0. Liverpool wakawa wapo nafasi ya kwanza. Mchezo uliofuata Liverpool walihitajika kushinda mchezo huo dhidi ya Palace, cha ajabu wakalazimishwa sare na kupoteza ubingwa.

Msimu huu Liverpool ipo moto, Chelsea haina kocha mzoefu sana, City wanasuasua, Arsenal haieleweki eleweki, Man United samahani siwezi kuizungumzia, hivyo ni fursa kubwa sana kwao kuwa bingwa mtarajiwa. Klopp ni mwalimu mzuri sana. Ana weledi wa hali ya juu katika taaluma hii. Naye pia ana matatizo yake binafsi ya utwaaji mataji. Swali ni je, mzimu wao unaishi au umeshakufa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here