Home Kimataifa KMC mkiukwepa Usimba na Uyanga Mtakua Kama KCCA

KMC mkiukwepa Usimba na Uyanga Mtakua Kama KCCA

4082
0

Makala na Raphael Lucas
Timu ya Manispaa ya kinondoni KMC ni moja ya klab zilizotokea kua tishio kwa hivi sasa ikiwa chini ya alowahi kua kocha wa Mbao fc ya Mwanza Etiene Ndayiragije ikishika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara wakijikusanyia jumla ya pointi 34,

KMC imeanza fanya vizuri sana hasa huu mzunguko wa pili huku ikitoa vichapo vya mbwa mwitu ni hili limechagizwa na ujio wa mshambuliaji Charles Ilanfya pamoja na uwiano mzuri wa akina James Msuva na upambanaji wa mabeki Kama Ally Ally na Ndikumana huku wakiwa na kipa mzoefu Kama Juma Kaseja,

KMC Naweza ifananisha na KCCA ya Uganda hii ni kutokana na aina ya umiliki na uendeshaji wake kua na chini ya mamlaka za kiserikali, ni vizuri kua na klab nyingi zenye ushindani hapa Tanzania kwani inasaidia kuongeza ushindani wa kimichezo hasa ili kutengeneza timu bora ya taifa leti

KMC wana mtihani mzito wa kukwepa Usimba na Uyanga kwenye uendeshaji na aina ya usajiri wanaofanya, club nyingi hapa nchini zimeshindwa kulikwepa tatizo hili kubwa ambalo club nyingi zimekua zikiingia huko na kushindwa kutoka kwenye hili dimbwi kubwa la umaskini wa kimawazo na kiuendeshaji.

Pamoja na hayo club inabidi impe mwanya mkubwa kocha katika kufanya maamuzi na kuitengeneza timu kiushindani zaidi, imekua ni mtihani mkubwa kwa club hasa zinazopanda ligi kuu Tanzania bara zinapofanya vizuri msimu wa kwanza kuja kua na mwendelezo wa matokeo hayo, cha msingi ikiwa KMC wataamua kufanya mambo yao kwa makini zaidi nategemea kuwaona levo za KCCA ya uganda.

KMC shitukeni mapema nazani nimeeleweka vizuri

Raphael Lucas(udom)
0710690782/0764764449

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here