Home Kitaifa KMC vs Mbao ni vita ya heshima

KMC vs Mbao ni vita ya heshima

3735
0

Ebwana eeeh KMC vs Mbao FC ni game kubwa, kali, tamu lakini haizungumzwi sana labda kwa sababu sio timu zenye mashabiki wengi.

Utamu wa game hii unatokana na kufahamiana vyema kwa timu zote na hii inatokana na KMC #KinoBoys kuchukua sehemu ya benchi la ufundi na baadhi ya wachezaji kutoka Mbao FC #Wabishi.

KMC ni timu inayocheza ligi kuu kwa mra ya kwanza katika historia lakini imembeba aliyekuwa kocha wa Mbao Etienne Ndayiragije ambaye ameambatana na aliyekuwa kocha msaidizi na meneja wa Mbao.

BECHI LA UFUNDI TOKA MBAO➡KMC
Kocha-Etienne Ndayiragije
Kocha Msaidizi-Ahmady Ally
Meneja-Faraja Moya

Kama vile haitoshi KMC wakafumua kikosi cha kwanza cha Mbao kwa kuwasajili wachezaji watano (6) muhimu kutoka Mbao ambao walikuwa wanategemewa.

WACHEZAJI TOKA MBAO➡KMC
Emanuel Mvuyekure
Yusuf Ndikumana
Sadala Lipangije
George Sangija
Kelvin Kijili
James Msuva

MBAO YAMUAPIA NDAYIRAGIJE

Kabla ya msimu kuanza nilifanikiwa kufika makao makuu ya Mbao FC pale mitaa ya Sabasaba-Mwanza wakati timu hiyo ilipokuwa ikitambulisha wachezaji kwa ajili ya msimu huu.

Mbao walitangaza timu 5 ambazo hawataziruhusu ziwafunge kwa namna yoyote ile nazo ni Simba, Yanga, Singida United, Alliance na KMC.

Wana sababu zao kwa nini hawatakubali kufungwa na timu hizo na tayari ‘Mnyama’ alichezea kichapo pale Mwanza. Mbao haitaki kufungwa na KMC kwa sababu Ndayiragije amewakimbia na wanataka kumfundisha adabu.

Mbao wanasema kufungwa na Ndayiragije ni aibu na dharau kwao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here