Home Kitaifa Kocha Mbeya City aeleza sababu ya vipigo ligi kuu

Kocha Mbeya City aeleza sababu ya vipigo ligi kuu

7520
0

Baada ya kupoteza mechi 3 mfululizo ugenini, timu ya Mbeya City inaendelea na maandali ya mchezo wake dhidi ya Alliance.

Kocha mkuu wa Mbeya City Ramadhani Nsanzurwimo ameeleza sababu za kupoteza mechi tatu za kwanza za ligi kuu Tanzania bara.

“Tulipoteza meche zetu 3 za kwanza, zilikuwa mechi ngumu kumbuka tulicheza na mabingwa wa ligi (Simba), tukapoteza na Azam (washindi wa pili wa ligi) katika mchezo wetu na Azam golikipa wao ilibidi apewe kadi nyekundu lakini aliendelea kucheza uamuzi haukuwa sawa.”

“Kinyume na hapo tulikuwa na matatizo kidogo, ndio tulikuwa tumetoka nyumbani hatujaingia vizuri kwenye ligi wakatumia makosa ya mtu mmoja mmoja. Mchezo dhidi ya Simba ulikutanisha wachezaji wenye uzoefu dhidi ya wasio na uzoefu. Hizo mechi mbili zilitupa picha kuelekea mchezo wetu dhidi ya Mtibwa tukijua tutashinda.”
::
“Tulipocheza na Mtibwa mechi ilikuwa nzuri lakini tulijipanga vibaya nyuma wakawa wanacheza mipira mirefu na kukimbia wakatufunga goli na goli lingine lilitokana na mpira wa kona.”

Mbeya City ilifungwa 2-0 na Azam mabingwa wa Kagame Cup 2018, ikapoteza mchezo wa pili kwa kufungwa 2-0 na Simba ambao ni mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara 2017/18 huku wakipoteza 2-1 mbele ya mabingwa wa FA Cup Mtibwa Sugar.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here