Home Dauda TV Kocha wa Simba apagawa Mwanza

Kocha wa Simba apagawa Mwanza

11727
0

Kocha wa Simba Patrick Aussems amesema nahodha John Bocco na Shomari Kapombe ni wachezaji pekee ambao wataukosa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sugar kwa sababu wana majeraha.

“Wachezaji wengine wote wapo vizuri tayari kwa mchezo na ninaamini wataonesha kiwango kizuri. Tunataka kushinda kila kombe katika mashindano tunayoshiriki tukianza na kesho”-Aussems.

Aussems amepagawa baada ya kukuta mamia ya washabiki wa klabu hiyo uwanja wa ndege wa Mwanza kwa ajili ya kuwapokea wachezaji waliokuwa wakitokea Arusha.

Aussems amesema anashangazwa na mashabiki wa Simba, kila sehemu wapo tena kea idadi kubwa tofauti na alivyokuwa anagikiria mwanzo kwamba mashabiki wengi wapo Dar pekeyake.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here