Home Kitaifa Kocha wa Yanga kwenda kwao Congo baada ya kuivaa Rayon

Kocha wa Yanga kwenda kwao Congo baada ya kuivaa Rayon

10966
0

Na Tima Sikilo

KOCHA mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ‘Papaa’, anatarajia kuelekea nchini kwao Septemba 2 kwa ajili ya kuungana na timu ya Taifa ya DR Congo na kuelekea nchini Liberia kwenye mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu fainali za kombe la Mataifa Africa kwa wachezaji wa Ndani (Chan) zitakazofanyika Cameroon mwaka 2019.

Kikosi cha Yanga kimesafiri leo kuelekea nchini Rwanda kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano dhidi ya Rayon Sport ya nchini humo.

Timu hizo zitapambana kesho Jumatano katika mchezo wa mwisho wa Yanga wa michuano ya kimataifa. Yanga wapo kundi D wakiwa wa mwisho na pointi nne.

Akizungumza na mwandishi kocha huyo amesema baada ya mchezo Baada ya Yanga kucheza na Rayon, ataondoka kwenda kujiunga na timu yao Taifa ya Congo ambayo ina mechi na Liberia.

“Baada ya Yanga kucheza na Rayon, Rwanda nitaondoka kwenda kujiunga na timu ya Taifa ya Congo ambayo ina mechi na Liberia kuwania kufuzu fainali za kombe la Mataifa Africa kwa wachezaji wa Ndani zitakazofanyika Cameroon mwaka 2019,” amesema Papaa.

Ikumbukwe kwamba Mwinyi Zahera pamoja na kwamba anainoa Yanga lakini vile vile ni kocha msaidizi wa kikosi cha timu ya taifa ya nchini Congo kama ilivyo kocha wa Singida United Hemed Moroco ambaye ni msaidizi katika timu ya taifa.

Wakati huo huo kocha ameongeza kuwa wachezaji ambao hawajasafiri na timu ni Papy Tshishimbi, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Saidi Makapu, Juma Mahadhi,Thabani Kamusoko na Amissi Tambwe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here