Home Kitaifa Kocha Mbeya City abwaga zigo kwa waamuzi

Kocha Mbeya City abwaga zigo kwa waamuzi

7139
0

Na Tima Sikilo

KOCHA mkuu wa timu ya Mbeya City, Ramadhan Nsanzurwimo amewatupia lawama waamuzi wa ligi kuu kwa kuwaambia wanatakiwa kusimamia haki na siyo kuchezesha kwa upendeleo.

Kocha huyo ametoa kauli hiyo baada ya pambano baina ya timu yake dhidi ya Azam FC ambapo walipoteza kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar.

Baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa ligi dhidi ya Azam FC, Nsanzurwimo amesema mwamuzi aliyechezesha mchezo wao hakutenda haki ndiyo sababu wameshindwa kurudisha hata bao moja.

Amesema wameyakubali matokeo lakini mwamuzi amefanya uonevu kwa kumwonyeshea kadi nyekundu mchezaji wao na kumuacha kipa Razack Abalora wa Azam ambaye naye alikuwa amefanya makosa.

“Kama mlivyoona mchezo tumecheza vizuri lakini waamuzi wanatuangusha kama waamuzi wataendelea hivi wataua soka letu,” amesema kocha huyo raia wa Burundi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here