Home Kitaifa Kuelekea msimu mpya: Kocha Mtibwa kazungumzia timu 20

Kuelekea msimu mpya: Kocha Mtibwa kazungumzia timu 20

7352
0

Kocha mkuu wa Mtibwa Sugar Zuber Katwila amesema, ligi ya Tanzania bara msimu huu itakuwa ngumu kutokana na idadi ya timu kuongezeka lakini pia itasaidia kuleta ushindanizaidi.

“Kwa mtazamo wangu, ligi kuwa na timu 20 ugumu utaongezeka kutokana na wingi wa timu lakini kiushindani zaidi itapendeza kwa sababu tutapata mechi nyingi za kucheza na rotation ya wachezaji itakuwa kubwa kwa sababu mechi zitakuwa nyingi”-Katwila amemwambia Peter Andrew.

Ratiba kupangulia

Awali ratiba ilielekeza Mtibwa ingecheza mchezo wa kwanza wa ligi kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro, lakini ratiba imebadilishwa na sasa watacheza ugenini (Dar) dhidi ya Yanga.

Siwezi kusema imeniathiri kwa sababu tulikuwa tunajiandaa kucheza ligi na pre-season tukijiandaa kucheza na timu 20, mabadiliko ya ratiba hayawezi kuniathiri, ni kitu cha kawaida tu kwa sababu hata usipocbeza nao sasa hivi utacheza nao baadae.

Tumetoka kucheza na Simba mechi ya Ngao ya Jamii kama ufunguzi wa ligi mechi inahofuata na Yanga ni timu kubwa vilevile lakini tumejiandaa kwa hilo, wachezaji wetu akilini mwao wanafahamu wametoka kucheza Simba wanakwenda kucheza na Yanga. Hakuna ugumu wowote kama umejiandaa kukabiliana na kitu kama hicho.

Nditi hakhonekana mechi za pre-season

Nditi hakuwa na matatizo kiufundi isipokuwa alikjwa na matatizo ya kifamilia vilevile alikuwa na program maalum tulimpa alikuwa akiifanya pekeake tofauti na wenzake kwa hiyo tutakuwa nae katika mechi zote za awali.

Nafasi ya Mtibwa Sugar kwenye ligi msimu huu

Lazima niipe nafasi kubwa kwa sababu timu yangu haijaondokewa na wachezaji wengi, ukiangalia asilimia kubwa ya watu wapo na ukiangalia wachezaji walioingia ni wachache wanne au watatu. Nafikiri tunaweza kukaa nafasi nzuri zaidi kuliko msimu uliopita.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here