Home Kimataifa Kuelekea “UEFA SUPER CUP” , Gabi anamshangaa Courtois wakati kuna hawa wasaliti...

Kuelekea “UEFA SUPER CUP” , Gabi anamshangaa Courtois wakati kuna hawa wasaliti wengine

13156
0

Thibaut Courtois hii leo hana uhakika wa kukaa langoni kwani bado hajacheza mechi hata moja Real, lakini Courtois kukaa langoni inaweza kuwa jambo chungu kwa mashabiki wa Atletico Madrid akiwemo nahodha wao aliyepita Gabi.

Gabi ameshangazwa na kitendo cha Courtois kujiunga na Real Madrid na anasema wazi imemuuma sana, kwani jambo hilo anaona kama sio fair kwa Atletico Madrid.

Hatuna uhakika nani ataanza na nani atakaa benchi lakini kupitia DSTV tutaona mambo yote hayo hii leo na kupata jibu. Kumbuka DSTV unaweza kuipata kwa laptop yako, simu au tablet ukidownload application yao.

Courtois alikaa katika lango la Atletico Madrid na kuichezea klabu hiyo michezo 111 ya La Liga lakini hii leo atakuwa katika upande wa pili wa majirani/wapinzani wao wakubwa Real Madrid.

Kwa Atletico Madrid mashabiki wake kama ilivyo Gabi huwa wanawachukia sana watu wanaohamia Real Madrid, lakini vivyo hivyo kwa Real Madrid sasa hawa hapa ni baadhi ya wasaliti maarufu.

1. Raul Gonzalez. Raul alikuzwa na kituo cha soka cha Atletico Madrid tangu mwaka 1990 lakini 1992 akahamia timu ya vijana ya Real Madrid huku 1994 akisainiwa timu ya wakubwa, michezo 132 aliichezea Real Madrid akifunga mara 66 na akabeba Champions League tatu na La Liga sita.

2. Juanfran. Juanfran yeye alikulia Real Madrid kuanzia 2003 akicheza mechi 62 na na mabao 7 kabla hajatolewa kwa mkopo Espanyol 2005 lakini ilipofika 2011 alisaini Atletico Madrid na hii leo ataiongoza kuwakabili Real Madrid.

3. Santiago Solari. Aliwasili Atletico mwaka 1999 akitokea River Platez kwa bahati mbaya msimu wa kwanza tu Atletico wakashuka daraja akatimkia Real Madrid akabeba La Liga mbili lakini pia alikuwepo dakika zote 90 fainali ya Champions League 2002, 2003 alienda Inter akarudi 2013 na sasa ni kocha wa wachezaji wa akiba.

4. Hugo Sanchez. Alinunuliwa Atletico 1981 akitokea Mexico na akawafungia Atletico mabao 52 katika mechi 111 na msimu wa 1984/1985 akawa kinara wa ufungaji La Liga, msimu uliofuata akajiunga Real Madrid huku akabeba tuzo ya ufungaji bora mara nne na akiwa Madrid alifunga mabao 164 kwenye mechi 207.

5. Bernd Schuster. Sasa raia huyu wa Ujerumani alikipiga Barca, Real na Atletico Madrid. Alianza Barca mwaka 1980-1988, ndipo Real Madrid wakamnyakua akwafunga mabao 13 michezo 61, baadaye akaenda Atletico Madrid mwaka 1990 akicheza mechi 85 na kufunga mabao 11, kabla ya kurudi kwao Ujerumani kuichezea Leverkusen.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here