Home Kitaifa “Kuna faida kubwa kuwa na kocha mwenye jina kubwa”-Haji Manara

“Kuna faida kubwa kuwa na kocha mwenye jina kubwa”-Haji Manara

9887
0

Mchezaji wa zamani wa Nigeria Emmanuel Amunike ametangazwa rasmi kuwa kocha mpya wa timu ya soka ya Taifa ‘Taifa Stars’ pamoja na timu za taifa za vijana kuanzia jana Jumatatu August 6, 2018 kwa mkataba wa miaka miwili ambao unaweza kuongezwa.

Haji Manara amesema kuna faida kubwa ya kuwa na kocha wa timu ya Taifa mwenye jina kubwa kwenye ulimwengu wa soka kama Amunike.

 

“Kuna faida kubwa kumchukua kocha mwenye jina kubwa kama Emmanuel Amunike, moja ya faida hizo ni macho ya mawakala yatakuwa yanaitazama Tanzania”-Haji Manara.

“Amunike ni jina kubwa sana, mechi yake kubwa ya kwanza akiwa na timu ya taifa ya Nigeria ni fainali ya AFCON Nigeria ilipocheza na Zambia mwaka 1994.”

“Katika fainali za mwaka huo Amunike hakuwa amecheza mechi zote kabla ya fainali, mchezo wa fainali Amunike akapangwa na akafunga magoli yote mawili kwa mguu wa kushoto Nigeria ikashinda ubingwa.”

“Kwa hiyo ni mchezaji kocha mwenye jina kubwa enzi za uchezaji wake. Ana faida kubwa, kuwahi kucheza Barcelona, kutoka kwenye nchi yenye jina kubwa kwa soka la Afrika kwa hiyo hata atakapo waamboa watu mchezaji fulani ni mzuri hakutakuwa na mashaka.”

“Tumpe muda na kumpa ushirikiano, inawezekana akawa na kitu kizuri. Jambo jema ni kwamba, ni kocha wa kiafrika kwa hiyo anajua mazingira ya Afrika.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here