Home Kimataifa Kuna Mo Salah Mmoja tu Afrika

Kuna Mo Salah Mmoja tu Afrika

4505
0

Maisha katikati ya mji wa Gharbia nchini Misri hayakumpa nafasi ya kuishi katika ndoto zake, alipanda daladala zaidi ya tano ili tu kuweza kufika katika uwanja wa kufanyia mazoezi huku shuleni akionekana kama mwanafunzi asiyejua alifanyalo alipitia mengi magumu ,kabla hajaitwa salah magoli kabla hajabatizwa jina la messi wa Africa.

Kila alichokuwa akifanya kilihusu mpira mawazo yake hayakumuwaza sana Isaac Newton kama baba yake alivyokuwa anafikiria kichwani kwake alimwona Mohamed aboutrika katika uhalisia wa maisha yake zaidi ya yule mwalimu wa soma la hisabati.

Aliamini ili njia itwe njia lazima isafishwe hakuwa sehemu ya majani katika ndoto zake hata tiketi ya ndege ya kwanza kwenda ulaya ilitokana na jasho lake alilovuja pale kwa farao kufika klabu ya Fc basel iliyopo Uswisi. Aliamini juhudi na kuzingatia kile kinachotolewa na kocha ndo msingi wa mafanikio zaidi.

Akatumia mda mwingi kufanya kile alichotumwa kukifanya hayo yalimfanya salah awe tunda la mzabibu ndani ya timu kubwa Ulaya, akafanikiwa kutua chelsea ambako alipita kipindi kigumu alionekana wa kawaida sana wengi walijuliza alifuata nini ulaya maana kwa kiwango chake hata ndani ya klabu ya Zamalek ya Misri asingeweza kupata nafasi.

Hakukata tamaa kwani maisha aliyopitia nyuma yalikuwa magumu kuzidi ya pale Stanford bridge akaaga na kwenda zake Italy.

Alitumia mda mwingine kujiuliza nini kilikosekana katika miguu yake katika klabu ya chelsea,akiwa katika klabu ya Fiorentina kwa mkopo ni kama alianza kuzifanyia kazi zile kanda za video za kina Maradona Ronaldo de lima alizokuwa anatazama zaidi ya kazi za mwalimu alizokuwa anapewa kipindi akiwa na umri wa miaka sita tu.

Maisha yakabadilika sana kwake akawa si salah yule tuliyemfahamu huyu alikuwa tofauti sana si tofauti ya wingi wa ndevu zake bali hata katika kutumia vizuri kilichopo katika miguu yake,akarudisha ile ladha yake halisi.

Liverpool wakamchukua hukutaka kwenda sehemu nyingine zaidi maana katika roho yake aliamini ndo wakati sahihi wa kuwaonyesha waingereza kuwa yeye ni nani
Ndani ya Liverpool lugha aliyofika nayo ilikuwa lugha ya mabao kila mechi hakuonekana kupungua kasi yake ya kufunga, magoli 36 ndani ya msimu mmoja unasimamaje pembeni yake.

Ndani ya misimu miwili Mo Salah amefanikiwa sana ndani ya Liverpool amegeuka injini ya timu kila anayeenda mbele katika kushambulia anamtizama salah yuko wapi.

Liverpool sasa kazi ngumu ni kuhakikisha mpira unafika kwake maana baada ya hapo kila tendo linalofanyika katika miguu yake linaacha alama katika kamera za wazungu
Kwa sasa Mo Salah yuko daraja la juu sana ukilinganisha na wachezaji wengine wa sasa wa afrika namna ya uchezaji wake usiohitaji mwili wa urefu wa futi sita wa peter crouch ama mwili wa kilo 84 wa didier drogba kubadilisha pasi kuwa goli.

Huhitaji kuudanganya moyo wako kuamini kuna mchezaji wa afrika anaeyemkaribia salah kiuwezo maana ni takwimu pekee zake bora uwanjani zinazomfanya aonekana kama anaishi bara lingine ndani ya afrika .
Hana mpinzani katika kuzichukua tuzo za afrika. Kwenye kabati lake la tuzo anatakiwa azidi kuliongeza maana tuna wachezaji na tuna mo salah mmoja tu katika bara la Africa

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here