Home Kitaifa Kuna usalama Singida United?

Kuna usalama Singida United?

2172
0

Benchi la ufundi la Singida United kutoelewana kunazua maswali mengi, utovu wa nidhamu? Kutoheshimiana? Kudharauliana? .
.
Kocha mkuu wa Singida United Dragan Popadic alikuja na msaidizi wake Dusan Momcilovic, Minziro aliipandisha timu lakini baadaye wakamtimua, wamemrudisha tena sasa wakati wa mchakato wa kumrudisha Popadic aliridhia?
.
.
Inawezekana Minziro alirudishwa tu kiaina kwa hiyo Popadic anashindwa kushirikiana naye kwa sababu tayari yeye alikuja na msaidizi wake na walimkuta Nsajigwa pale. Au Singida United ndio timu yenye benchi la ufundi lenye wataalam wengi ligi kuu Tanzania bara?
.
.
Kuna mambo mengine timu zetu zinafanya ayaendani na mpira wa kisasa, kuleta kocha mkuu ametoka huko na msaidizi katoka kule mwisho wa siku unatengeneza benchi la ufundi ambalo kila mtu anaamini tofauti na ana falsafa zake.
.
.
Baada ya Hans van Pluijm kuondoka Singida United, Hemed Suleiman ‘Morocco’ alitangazwa kuwa kocha wa timu hiyo, hakudumu sana akaondoka akamwacha msaidizi Jumanne Chale lakini badaye akaongezwa Shadrack Nsajigwa.
.
.
Chale akaikimbia timu na kumwacha Nsajigwa baadaye wakaletwa wazungu (Popadic na Dusan) timu ikaendelea kufanya vibaya Minziro amerudishwa, kuna usalama Singida United? Au watu wameshaona timu inashuka daraja wanamalizia siku?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here