Home Kimataifa Kutoka 32 hadi 13 Dani Alves abadili namba ya jezi, sababu ni...

Kutoka 32 hadi 13 Dani Alves abadili namba ya jezi, sababu ni Mario Zagallo

9026
0

Unamjua Mario Zagallo? Kwa taarifa yako huyu ndiye mwanadamu wa kwanza kushinda kombe la dunia kama mchezaji lakini baadae akaja kushinda akiwa kama kocha.

Mwaka 1958 na 1962 alishinda akiwa kama mchezaji wa Brazil, lakini mwaka 1970 na 1994 akashinda tena kombe hilo akiwa kama kocha (1994 alikuwa msaidizi).

Katika vitu ambavyo Zagallo alikuwa akiviamini kuhusu mafanikio yake katika soka haswa wakati akiwa mchezaji ni bahati, na anaamini jezi namba 13 ina bahati kubwa katika soka.

Sasa mlinzi wa kulia wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Dani Alves ameamua kufuata nyayo za Zagallo kwa kuomba kupewa jezi namba 13 akiwa na PSG.

Awali Alves alikuwa akivaa jezi namba 32 lakini sasa akitoka kwenye majeruhi atakuwa akivaa namba 13, huku yeye mwenyewe akisema anavaa jezi hiyo kutokana na namna Zagallo alivyomhamasisha kujituma na kufika hapo alipo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Alves amesema sio tu kumkubali au bahati bali Zagallo amefanya mengi katika mpira wa taifa lao na hivyo anahitaji kupata heshima kubwa kutokana na hilo.

Kama haujui tu ni kwamba Alves sio nyota wa kwanza kuvaa jezi namba 13 kwa siku za karibuni kwani Thomas Muller, Michael Ballack, Maicon na hata Gerd Muller ambaye ndio mwanadamu wa kwanza kufikisha mabao mengi (14) kombe la duna(1970(10) na 1974(4)) alikuwa akivaa namba 13.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here