Home Kitaifa Kutoka kwenye kuuota “usoja” hadi sasa anaiota EPL, Samatta na ndoto zake

Kutoka kwenye kuuota “usoja” hadi sasa anaiota EPL, Samatta na ndoto zake

13042
0

Kama ulikuwa hujui hii ndio fursa ya wewe kujua, nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta kupitia post yake kwenye mtandao wa Instagram amefunguka kuwa, kabla ya soka alikuwa anatamani kuwa mwanajeshi.

Samatta ame-post picha akiwa ndani ya uzi wa Stars picha flan ambayo yupo serious sana kisha akaandika: “Muda mwingine Mungu hakupi unaloliomba ila anakupa linalokustahili…kabla ya soka nilikuwa natamani kuwa mwanajeshi, je kwa sura hii unadhani ningestahili kuwa soja?

Sawa ndoto ya usoja imekufa, kwa sasa unaota nini?

Naitamani EPL” Katika dirisha la usajili lililofungwa hivi karibuni barani Ulaya, kulikuwa na taarifa kuhusu vilabu kadhaa kuhitaji huduma ya Samatta, Mwenyewe amesema kulikuwa na klabu nyingi ambazo zilihitaji huduma yake lakini hakuwa tayari kutaja vilabu hivyo kwa sababu tayari dirisha limefungwa.


Kulikuwa na vilabu vingi (siwezi kuvitaja ambavyo vinanihitaji lakini haikuwa bahati kwa wakati huo hadi dirisha linafungwa, kwa hiyo tusubiri dirisha lingine.

Mwisho wa siku Samatta amesema anamapenzi na ligi ya Engandi haijalishi ni timu gani atacheza lakini iwe ni ya ligi kuu

Mimi siku zote nina mapenzi na ligi ya England haitojalisha ni timu gani, yoyote ambayo inacheza ligi kuu sijali.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here