Home Ligi EPL Kwa Messi sawa, lakini vipi kuhusu Griezman na Varane kupotezewa na FIFA?

Kwa Messi sawa, lakini vipi kuhusu Griezman na Varane kupotezewa na FIFA?

9835
0

Tuzo ya mchezaji bora wa dunia ilianza kutoka mwaka 1991 ambapo mchezaji wa kwanza kushinda tuzo hiyo alikuwa ni Lothar Matthaus akiwa katika kiwango bora na Inter Milan lakini alitoka kuiongoza Ujerumani kushinda kombe la dunia akiwa nahodha.

Tangu mwaka 1991 tuzo hiyo ikifanyika katika mwaka ambao kombe la dunia limefanyika, walioingia fainali kuwania tuzo hiyo ilihusha wachezaji walitoka kwenye nchi iliyochukua ubingwa wa kombe la dunia.

Tuzo ya kwanza ambayo ilifanyika baada ya kombe la dunia ni ya mwaka 1994 ambapo wachezaji watatu walioingia fainali kuwania tuzo hiyo Hristo Stoichkov, Roberto Bagio na Romario na Romario aliibuka mshindi.

Bagio alifika fainali akiwa na Italy, Stoichkov alikuwa na msimu mzuri sana wa kombe la dunia na Bulgaria ambayo ikifika hadi nusu fainali. Romario alikuwa Barcelona mwaka 1994 chini ya kocha Johan Cruyff Barcelona iliyokuwa ikiitwa The Golden Era walikuwa wameshinda ubingwa wa La Liga na kufanya vizuri kwao.

Naamini Stoichkov alikuwa na msimu bora wa fainali za kombe la dunia akiwa mfungaji bora wa mashindo baada ya kufunga magoli matano.

Mwaka mwingine wa kombe la dunia ulikuwa 1998 ambapo Zinedine Zidane alishinda tuzo hiyo, wachezaji watatu walioingia fainali walikuwa ni Ronaldo de Lima alicheza fainali pamoja na Davor Sukar ambaye alikuwa mfungaji bora na timu yake ilitolewa na Ufaransa hatua ya nusu fainali.


2002 mwaka mwingine wa kombe la dunia, wachezaji waliokuwa wanawania tuzo hiyo ni Zidane ingawa Ufaransa ilitolewa mapema kwenye kombe la dunia lakini alikuwa amefanya vizuri kwenye Champions League na kuisaidia Madrid kushinda ndoo baada ya kufunga goli katika mchezo wa fainali dhidi ya Liverkusen. Oliver Kahn alicheza fainali ya kombe la dunia dhidi ya Brazil panoja na Ronaldo ambaye timu yake ilishinda ubingwa huo, Kahn na Ronaldo walifanya vizuri kombe la dunia Zidane alifanya poa Champions League.


Mwaka 2006 Fabio Cannavaro akiwa na Italy mabingwa wa dunia mwaka huo ndio alishinda tuzo lakini alikuwepo Zidane ambaye alicheza fainali na Ronaldinho ambaye alibebwa na Champions League kwa sababu mwaka huo Barca walikuwa mabingwa baada ya kumfunga Arsenal lakini kwenye kombe la dunia Brazil walitolewa na Ufaransa hatua ya robo fainali.

2010 alikuwepo Andres Iniesta na Xavi ambao walishinda ubingwa wa dunia, Messi aliingia licha ya Argentina kutolewa robo fainali ya kombe la dunia, upande wa Champions League kombe lilienda Inter Milan, mwaka huo tuzo hii iliibua mijadala mingi sana baada ya Messi kushinda.

Cristiano Ronaldo akashinda tuzo hiyo mwaka 2014 Madrid walikuwa mabingwa wa Champions League mwaka huo lakini kwenye kinyang’anyiro alikuwepo Manuel Neuer mshindi wa kombe la dunia alikuwepo pia Messi wakati huo Argentina ikiwa imecheza fainali ya kombe la dunia.


Sasa mwaka 2018 wanaowania tuzo hiyo ni Modric amecheza fainali ya kombe la dunia, Ronaldo Ureno ilitoka mapema kombe la dunia lakini Madrid ilikuwa bingwa wa Champions League na Salah timu yake ya taifa ilitoka hatua ya makundi kwenye kombe la dunia lakini alicheza fainali ya Champions League akiwa na Liverpool.


Kwa miaka kadhaa ambayo nimeirodhesha hapo juu katika nominees watatu wa mwisho alikuwepo mchezaji ambaye ametoka kwenye timu iliyoshinda ubingwa wa kombe la dunia lakini mwaka huu ndio hakuna mchezaji kutoka kwenye timu bingwa wa kombe la dunia ndio maana hoja ya Antoine Griezmann inaibuka kwamba alistahili kuwepo kwenye orodha ya wachezaji watatu.


Ameshinda Europa League na kombe la dunia, sawa wamempotezea Griezmann kwa nini basi Raphael Varane asiingie kwa sababu ni mshindi wa Champions League na kombe la dunia na alikuwa miongoni mwa wachezaji bora kwenye mashindano yote.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here