Home Uncategorized Kwanini Chelsea walifungwa na Spurs?

Kwanini Chelsea walifungwa na Spurs?

7794
0

WAZO HURU: Makala na Roberto Komba

Jumamosi iiliyopita tulishuhudia moja ya tukio zuri katika soka na likiwa tukio baya kwa klabu ya Chelsea na mashabiki wake kwani walipata kipigo chao cha kwanza cha msimu kutoka kwa Tottenhma Hotspurs ya Mauricio Pochettino, kipigo cha mabao 3-1 kikisindikizwa na soka kubwa, kwa maelezo mafupi ni kwamba Chelsea walizidiwa katika sehemu kubwa ya mchezo kwani licha ya kuwa na umiliki wa mpira kwa zaidi ya asilimia 60%, lakini bado Chelsea walishindwa kuutawala mchezo na kuacha Spurs wakitawala mchezo pale ambapo walikuwa na mpira na hata walipokosa mpira na kujitengezea nafasi nyini zilizowawezesha kupata jumla ya mashuti 9 yaliyolenga lango. Nini kilitokea kwa Chelsea ambayo kabla ilifikisha michezo 12 bila kupoteza katika ligi?

KUZUIWA KWA JORGINHO
Pochettino kama makocha wengi ambao wamekutana na Chelsea msimu huu, alitambua fika kwamba mfumo wa uchezaji wa Chelsea almaarufu kama “sari-ball” unategemea kwa kiasi kikubwa uwezo wa kusoma nafasi na kupiga pasi wa Jorginho na hivyo kumzuia hasipate mipira mingi ni kuizuia Chelsea isitengeneze nafasi na kutawala mchezo, ndivyo walivyofanya spurs kwani kuanzia mshambuliaji wa kati (Harry Kane) na viungo washambuliaji (Son, Ericksen na Delle Alli)

wote walifanya pressing na kuzuia mipira isije kwa Jorginho mara kwa mara, na hata ilipofika basi Viuno wakabaji (sissoko na Dier ) walikuwa wa kwanza kuupata huo mpira, huku kwa nyakati tofauti wakitumia ukabaji wa mtu na mtu katika eneo la kiungo, kitu kilichowafanya Chelsea kubaki nyuma na kuamua kupitisha mipira pembeni, ingawaje licha ya kufanya hivyo, Chelsea ilikosa nguvu ya kutawala mchezo ikiwa na mpira, ili lilithibitika kwa Jorginho kumaliza mchezo akiwa na pasi 43 tu zilizofika, licha ya kuwa na wastani wa zaidi ya pasi 90 kwa mechi hapo kabla.

KUWEPO KWA UWAZI KATIKA ENEO LA MBELE YA MABEKI

Kimsingi hili limekuwa ni tatizo la Chelsea msimu huu licha ya kuwa na rekodi nzuri, kumekuwapo na uwazi katika eneo la mbele ya mabeki hasa wakati wa kipindi cha mpito (transition) kuelekea kuzuia, kwani mara nyingi Jorginho husogea juu timu ikiwa na mpira na sio mchezaji mwenye kasi sana hivyo kuchelewa kurudisha mpira na timu nyingi zimejaribu kulitumia hilo ombwe ikiwa pamoja na Liverpool katika mechi iliyofanyika stamford bridge ambapo Sturridge akiwa katika eneo hilo alipia shuti lililomshinda golikipa Kepa Arrizaballaga na kufanya matokeo kuwa 1-1, lakini Pochetino aliitumia kosa hilo kwa ufanisi zaidi kwani mara nyingi sana Spurs walionekana kukimbia katika eneo hilo na kulishambulia ipasavyo na kuwaacha Chelsea wakiwa waanga, kwa mara nyingine kwani Harry kane alipia Mpira mrefu uliojaa kimiani akiwa katika eneo hilo.

UWAZI KATIKA MAENEO YA PEMBENI HASA KUSHOTO

Hili pia ni moja kati ya tatizo la Chelsea kwa msimu huu, kwani kocha Maurizio sari hupenda kuwaelekeza mabeki wake wa pembeni kusoea juu sana wakati wa kushambulia ili kutoa mapana (width) na akiwataka viuno wa pembeni (Kante upande wa kulia na Kovacic/Barkley kushoto) kusaidia kurudisha mpira ukiwa umepotea wakati ambapo beki wa kushoto huwa eneo la juu, bahati katika upande wa kulia ambapo kuna mabeki cesar Azpilcueta na kiuno Ngolo Kante ambao wana kasi na hivyo huwa halidhuriki sana lakini katika upande wa kulia ambapo Chelsea hupenda sana kutumia katika kushambulia, beki Marcos Alonso hana kasi sana na imekuwa chanamoto kwa Chelsea na hata spurs walijariu mara nyini kutumia udhaifu huo kwani mara nyini katika mashambulizi ya kushtukiza walijaribu kulitumia eneo hilo na mwanzo kabisa wa mchezo wakapata faulo upande huo na ilizaa goli la kwanza.

HITIMISHO
Chelsea imekuwa bora na kama timu nyini ambazo zimeinia katika mfumo mpya chini ya kocha mpya, nayo imehanaika sana kufikia utimilifu na spurs ni moja kati ya timu nzuri sana ulimwenuni, kwani kocha wao Pochettino amethibitisha kuwa mbunifu mzuri wa mbinu na timu yake kutokana na kukaa mda mrefu pamoja, inajua nini cha kufanya katika kila hatua ya mchezo, inawaje kocha wa Chelsea alielezea kabla na hata baada ya mchezo kuwa timu yake ina tatizo la kisaikolojia la kuanza mechi vibaya na kushika kasi baada ya dakika 20 za mwazo.

Kitu ambacho kilidhihirika katika mechi hiyo lakini zaidi ya yote mbinu za Pochettino zilithibitika kuwa bora na kufanya kazi kama zilivyotarajiwa

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here