Home Kitaifa Kwanini makocha wengi wanapendelea sana mfumo wa 4-4-2

Kwanini makocha wengi wanapendelea sana mfumo wa 4-4-2

3822
0

“Kwanini 4-4-2 kila siku?” Ndio swali ambalo Nina mpango wa kuwauliza makocha takribani 18 kati ya 20 wa timu zinazocheza ligi kuu Tanzania bara na makocha wengine zaidi ya 30 wa timu za daraja la pili katika kikao cha kufukirika kitakachifanyika kwenye sehemu ya kuchezea ya uwanja wa taifa.

Ni swali ambalo nitawauliza wadau wa soka katika kigoda cha mwalimu Nyerere (michezo) kwenye ukumbi wa Nkurumah pale chuo kikuu cha Dar es salaam.

Nitasikiliza kwa umakini mkubwa majibu ya wadau kwa kuwa hili ndio swali ambalo napenda kujiuliza zaidi. Wakati nikijaribu kujiuliza kwanini tumekuwa na kasi ndogo katika ukuaji wa soka. Yamkini wadau wengi katika kikao hicho watataka kujadili masuala kama rushwa michezoni, uongozi mbovu, kukosekana kwa vyuo vya soka kwa vijana na utovu wa nidhamu kwa wachezaji kama ndio sababu kuu kwa kasi hiyo ndogo ya ukuaji wa soka.

Lakini sitasita kuwakumbusha kuwa wanasahau; mfumo/muundo wa 4-4-2 ambao unachochea mipira mirefu ni sababu kubwa tu katika hilo. Lakini labda hoja yangu kubwa haitakuwa mfumo wa 4-4-2 pekee. Bali ni kile kinachoashiriwa kwa kuzidi kwa utumizi wa mfumo huo. Nitawaeleza mawazo yangu ya kuwa mfumo huo unatuelezea kwa kina falsafa ya mpira uliopo nchini, na ni rahisi kuona matokeo yake katika timu ya taifa. Timu yetu ya taifa kwa mtizamo inacheza kama ambavyo timu zetu nyingi za ligi kuu zinavyocheza, japo muundo unaweza kubadilishwa na makocha Lakini wachezaji wetu Mara nyingi wanatuonyesha kile kile tunachokiona katika 4-4-2.

Mpira wetu unaweza kutafrika kama mpira uliotawaliwa na mipira mirefu, utumizi wa nguvu na mfumo wa 4-4-2. Yamkini labda kuna watakaonijibu kuwa mfumo huo ni rahisi kufundisha na kueleweka kwa wachezaji. Hoja yao ni sahihi lakini nitawaambia kuwa hayo ni mapokeo, walimu wanafundisha walichopokea na wachezaji wanapokea wanachofundishwa na walimu. Ugumu na urahisi ni sio dhana ya wazi Bali ni fikra za wahusika.

Lakini pia ntawaeleza jinsi 4-4-2 inavyoweza kupunguza fursa ya kuwa na umiliki mkubwa wa mipira uwanjani, kitu ambacho ni silaha kubwa ya mpira wa sasa, 4-4-2 inafanya nafasi zinazotengenezwa ziwe za namna inayofanana na hivyo kufanya mchezo utabilike na kuwa rahisi kuukabili, kama ambavyo tunaweza kuona hali hii ikidhihirishwa kwa ufinyu wa mabao katika mechi zetu, matokeo ya 1-0, 0-0 , 2-0 ama 2-1 yameutawala sana mpira wetu.

Ntahakikisha naondoka nikiwa nimetoa duku duku langu na nikiacha mchango chanya katika mabadiliko ya mbinu za soka nchini, kwani Nina imani wataondoka kikaoni wakiwa wanajitafakari na kutafuta sio tu ‘muundo’ Bali hata mbinu za kuondokana na haya niliyowaambia. Kwani lengo ni kutaka kujaribu na kuweka dhana ya kucheza aina bora zaidi ya mpira na kuondoka na visingizio kama ubovu wa uwanja. Nitawaambia kuwa ni bora tuone makosa yanayotokana na viwanja vibovu yakisababisha magoli, kuliko kuona mechi mechi 290 kati ya 300 za msimu zikichezwa kwa soka lililochezwa mwaka 1967.

Imeandaliwa na Robert Komba
Robbiekomba@gmail.com
0762283468

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here