Home Kimataifa Legend wa Afrika afariki Sauz

Legend wa Afrika afariki Sauz

3300
0

Mkongwe wa DR Congo na soka la Afrika kwa ujumla Mulamba Ndaye [katikati aliyeshika jezi ya Zaire (DR Congo)] amefariki nchini Afrika Kusini akiwa na umri wa miaka 70.

Strike huyo wa zamani alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya moyo pamoja na figo muda mwingi alikuwa akitembea kwa msaada wa kiti maalum cha wagonjwa ‘wheelchair’.

Anaendelea kushikilia rekodi ya kufunga magoli mengi kwenye mashindano ya mataifa ya Afrika (kwenye tournament moja) baada ya kufunga magoli tisa (9) na kuisaidia Zaire wakati huo kutwaa ubingwa wa pili wa mashindano hayo mwaka 1974 nchini Misri ambapo pia walifuzu kucheza fainali za kombe la dunia nchini Ujerumani.

Ndaye aliiongoza timu yake ya taifa akiwa nahodha kwenye mashindano ya kome la dunia 1972 ambapo alitolewa kwa kadi nyekundu (iliyozua utata) kwenye mchezo wa pili dhidi ya Yugoslavia.

Aliichezea AS Vita Club ya DR Congo kwa miaka 16 hadi akiwa na umri wa miaka 38 na kuisaidia kutwaa ubingwa wa Afrika mwaka 1973.

Kuna wakati alidhaniwa amefariki kwenye ajali ya mgodi mmoja huko Angola mwaka 1998 ambapo kabla ya mchezo mchezo kati ya DRC dhidi ya Burkina Faso watu walitoa heshima ya kukaa kimya kwa dakika moja kabla ya kuanza mchezo huo.

Baada ya kutunukiwa medali ya heshima na chama cha soka Afrika (CAF) mwaka 1994, baadaye alipigwa risasi mguuni na  watu wanne waliokuwa wamevalia sare za jeshi na walikuwa wakihitaji medali aliyopewa pamoja na fedha.

Akiwa na wasiwasi wa usalama wake, Ndaye alikimbilia South Africa ambako aliishi maisha ya kifukara kwa miaka mingi kwenye jiji la Cape Town.

Rest In Peace #Legend

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here