Home Ligi EPL Leicester City wataweza kuzuia moto wa Liverpool Jumamosi hii?

Leicester City wataweza kuzuia moto wa Liverpool Jumamosi hii?

8855
0

Mwanzo wa Leicester katika ligi unaonekana kuwa mzuri lakini Liverpool wameanza vyema zaidi mpaka baadhi ya watu wameanza kusema ndio timu ambayo inaweza kuizuia City wasitetee ubingwa wao.

Claude Puel, ambaye Jumapili hii inatimiza miaka 57, ana rekodi bora dhidi ya Liverpool: akifungwa mechi moja tu katika michezo 7, akiwa na Lyon, Soton na Leicester.

Lakini Puel atakuwa bila Jamie Vardy, na takwimu zinaonyesha kukosekana kwa Vardy ni jambo la faida sana kwa Liverpool. Vardy amefunga magoli 7 katika mechi 5 zilizopita vs Liverpool- magoli 7 hayo ni sehemu ya magoli 9 ya Leicester vs Liverpool.

Hali ya Vikosi – Jamie Vardy ataukosa mchezo huo kutokana na kusimamishwa mechi 3
Caglar Soyuncu bado anaendelea kuijenga fitness yake baada ya kuumia, wakati Matty James nae bado anasumbuliwa na enka.

Upande wa Liverpool, mlinzi Dejan Lovren bado hana utimamu wa kiafya kucheza mchezo wake wa kwanza wa msimu, anaungana na Alex Oxlade-Chamberlain kwenye listinya wachezaji wagonjwa wa Liverpool.

Head To Head Records

•Liverpool walimaliza uteja wa kupoteza mechi 3 mfululizo vs Leicester kwenye mashindano yote kwa ushindi wa 3-2 mnamo September 2017.

• Liverpool wameshinda mechi 8 kati ya 12 za ligi dhidi ya Leicester City.

• Majogoo wameshinda mechi 4 mfululizo za ligi bila kuruhusu wavu wao kuguswa – mara ya mwisho hili kutokea ilikuwa 2005.

• Kumekuwepo na kadi nyekundu 8 katika michezo ya EPL inayowahusisha Leicester City tangu mwanzo wa msimu uliopita, ni Everton pekee ambao wamewazidi kwa kadi nyekundu 11.

Mchezo huu utachezwa saa 8:30 mchana – live on DSTV pekee.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here