Home Ligi BUNDESLIGA Leon Bailey aliteseka sana kabla ya hajakutana na Samatta

Leon Bailey aliteseka sana kabla ya hajakutana na Samatta

16344
0

Kuna mwandishi mmoja anajulikana kama Marlon James aliandika kitabu cha A Brief History of Seven Killings kitabu chake kilikataliwa mara 78. Yupo kinda wa Kijamaica ambaye pia alisuswa sana na vilabu vingi vya Ulaya.

Leon Bailey Butler ( 9 Agosti 1997) kule nchini Jamaica. Kwa sasa yupo Bundesliga ndani ya klabu ya Bayer Leverkusen. Aina yake ya uchezaji naifananisha na ile ya Malcom aliyetimkia Barcelona. Huyu alikuwa swahiba mkubwa wa Samatta katika klabu ya KRC Genk.

Bailey alizaliwa maeneo ya Cassava Piece kule mjini Kingston, Jamaica.

Leon Bailey
Taarifa binafsi
Majina Leon Bailey Butler
Kuz 9 Agosti 1997 (20)
Mah Kingston, Jamaica
Kimo 1.81 m (5 ft 11 12 in)
Nafasi Winga

Kabla Bailey hajajiunga na Bayer Leverkusen alikataliwa sana na vilabu mbalimbali.

Hapo awali akiwa shule ya msingi alijiunga na shule ya vipaji ya Phoenix All-Stars Football iliyokuwa chini ya mzee Craig Butler ambaye baadae alikuja kuwa baba yake mlezi.

Licha ya kukataliwa mara kadhaa kocha Papine FC bwana Andrew James ni mmoja kati ya watu walioamini kipaji chake.

Akiwa na miaka 12 Leon aliweka rekodi ya kutwaa vikombe kadhaa (U13, U15 na U17 pamoja na kupewa zawadi ya MVP Mchezaji muhimu zaidi) pia alikuwa mfungaji bora mara mbili (U13 na U15).

Kutokana na kuonesha kiwango maradufu mzee Craig alimchukua Leon, Kyle na wachezaji wawili wa akademi Phoenix All-Stars Kevaughn Atkinson na Romario McKnight mpaka nchini Austria. Walikutana na aliyekuwa kocha wa vijana wa Ajax na PSV Percy Van Lierop. Wote wanne walifeli kwenye majaribio. Maisha yao yalianza kuwa magumu. Ulaya baridi kali uchumi wao ukaanza kuyumba kwa kasi sana. Mbaya zaidi walikwe da ulaya wakiwa na fulana na bukta tu huku baridi la Austria lilikuwa kali sana.

Takwimu zake za Bayerne Liverkusen

 1. Mwaka

  M

   G

  As

  2017-18

   30

   9

   6

   2

   0

  2016-17

  8

  0

  0

  11

  0

  Walipita kwenye wakati mgumu sana. muda wao wa majaribio pale Rapid Wien uliisha wakakosa sehemu ya kulala. Ilibidi wote kwa pamoja kulala nje karibu kituo cha Wien railway station.

  Mzee Butler anasema The Green-Whites walikataa kuendelea kuwalipia hela ya malazi na wakafukuzwa hotelini na kwenda kulala nje ya ukuta wa kituo hicho cha treni.

  Wachezaji wanne wale baadae walipata nafasi USK Anif. Kyle alipta nafasi ya kuwa nahoda wa timu ya U15, Leon alikuwa mshambuliaji na Atkinson alipata nafasi pia. Walishiriki michuano ya huko mjini Salzburg kwenye mashindano ya Regionalliga.

  Mzee Butler aliteuliwa kuwa skauti wa USK Anif, licha ya kwamba walikumbana na changamoto ya FIFA ya kusafirisha wachezaji wenye umri wa chini ya 18.

  Kikosi cha U15 klabu yao ya Anif walicheza dhidi ya Sportkulb Adnet wakatoa dozi ya mabao7-0 na Leon alitia kimya mabao matano. Mwisho wa msimu Leon alivurumisha mabao 75 kwenye 18 tu. Khaaa kweli huyu kijana alikamia.

  Baba yake akansa kufukuzia madili ya Ujerumani na Uholanzi ya vilabu vya Mainz na Ajax . Wakala mstaafu bwana Jimmy Floyd Hasselbank aliyekuwa mkurugenzi wa maskauti wa Mainz akawapigia simu akina Bailey. Wote wakaenda kufanya majaribio. Ni mchezaji mmoja tu aliyebakishwa na klabu hiyo nae ni Atkinson (alisaini mkataba wa miaka mitano na Bayern Munich, wakati huo pia walikuwepo wajamaika wengine walikuwa wakifanya majaribio vilabu vya Hamburger SV, SV Grödig and FK Austria WienDFB Pokal

  Mwaka

  M

  G

  As

   2017-18

   4

   3

   0

   1

  0

  Vijana hawa wawili Kyle na Leon mambo yao yakawa yanaenda mrama. Januari 2012 Ajax wakaanza kuwafukiza vijana hawa wa Kingston walioletwa ulaya na Butler, Butler alikuwa akitumia marufuku nchini kwake kwa akademi yake kufanya biashara haramu ya kusafirisha vijana wadogo na kwenda kuteseka ulaya kwa ajili ya kutafuta mwanya wa kuwika barani huko.

  Mzee Butler alikuwa ameishiwa kiasi kwamba ilibidi mali nyumbani kwake ziuzwe ili wapate nauli ya kuwasafirisha Kyle na Leon mpaka mjini Ajax. Mkurugenzi Ajax maarufu kama “The Lancers’” alipenda sana kasi ya Leon na hata uwezo wake wa kutulia na mpira. Kwenye kikosi cha watoto walimpachika jina la “Chippy”, baada ya kumfananisha na staa wa tamthiliya za “Alvin na Chipmunks”.

  Licha ya kukubalika sana ndani ya kikosi cha vijana Ajax waliogopa kumpa mkataba kwa kile walichohofia kupigwa penati kwa sababu vijana hao walionekana kama wazamiaji ulaya wala hawakuwa na nyaraka maalumu. Ikumbukwe kuwa baba yao alikuwa akifanya kazi kinyume cha taratibu za taifa lao hivyo hakupata msaada wowote kutoka Jamaica.Champions League

  Mwaka

  M

  G

  2016-17

  2

  0

  0

  0

  Mungu sio Athumani klabu ya Ubelgiji ikapata taarifa za hawa vijana klabu hiyo ni Racing Genk. Butler akamsihi mkurugenzi wa Ajax amsaidie nauli ya kuwapeleka vijana mpaka Ubelgiji.

  Leon alifanikiwa kupata nafasi katika klabu hiyo lakini kwa ndugu yake ilikuwa kama ndoto za mchana licha ya safari ndefu ulaya.

  Craig Butler, alienda mpaka Mexico akawaacha Leon na Kyle katika harakati za kujaribu kukwepa rungu la FIFA na mkono wa serikali yake. Alirudi baada ya miezi minne huku akidai kuwa alitekwa na kuibiwa kila kitu na watu wasiojukikna na waliomtishia maisha. Taifa la Ubelgiji likapata taarifa kutoka kwa vyombo vya usalama vya Jamaika kuwa watu hao hawapaswi kuajiriwa ndani ya taifa lao. Mkataba wa Leon nao ukafutiliwa mbali.

  Mkurugenzi wa ufundi wa Ajax akachukua uamuzi wa kuwasiliana na klabu ya Slovakia ya AS Trenčín, ambao walikuwa marafiki wakubwa wa Ajax tokea 2012.

  Leon na Kevin wakaanza kazi Trenčín.
  Meneja wa klabu hiyo Robert Rybnicek akajaribu kuwatafutia kibali cha kufanya kazi mpaka 2017. Hawakusaini mkataba wowote mpaka oale walipotimiza miaka 18 ambapo Leon na Kevin walijiunga na klabu ya Genk.

  Kwa bahati Genk wakakutana na Rapid Wien timu ambayo ilimnyima makazi hata sehemu ya kujilaza tu. Genk walipoteza kwa mabao 3-2 lakini Leon alifunga mabao yote mawili ya Genk ikiwa ni pamoja na bao lake murua kabisa.

  Chelsea sasa inamfukuzia kinda huyu ambaye sasa hivi hahitaji tena mechi za majaribio ili kuonekana. Nyota njema ilishaonekana tokea akiwa Genk alipotwaa tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa mwaka wa Jupiler Pro League mwaka 2015/2016

  Baada ya kiwango bora ndipo akatimkia zake Bayer Leverkusen. Klabu ya Genk pia wamepita nyota kama De Bruyne, Courtois, Origi, Milinković-Savić, Ferreira-Carrasco na Kalidou Koulibaly.

  Takwimu nyinginezo za msimu uliopita
  Leon Bailey 2017/18 Bundesliga:

  30 Mechi alizocheza
  25 Mechi alizoanza
  196 krosi alizopiga
  76 Mashuti
  59 Nafasi alizotengeneza
  58 Amewatoka mabeki kwa kasi
  9 magoli
  6 asisti

  🔥

  Pia Bailey amejizolea jina kubwa sana Jamaica. Lakini bado nafsi yake inachuki na utaifa wake ambalo lilimtenga tokea awali. Alipoulizwa kama anaweza kuhama taifa lake alisema ndio

  Mtu akiniambia nicheze Belgium, ndio nitakubali! napenda kushiriki michuano mikubwa na kucheza dhidi ya wachezaji nguli. Kwa upande wa Jamaica sioni fursa hiyo”

  Mimi ni Privaldinho

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here